Kundi la wafanyabiashara 15 kutoka Oman limewasili jijini Dar es Salaam ambapo inatarajiwa kuwa na mazungumzo na Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal nyumbani kwake, Oysterbay baada ya Uzinduzi wa Baraza la Biashara baina ya Tanzania na Oman.
Wafanyabiashara hao ambao wanakuja nchini baada ya kuvutiwa na fursa zilizopo nchini ambazo zilielezwa vema na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa ziarani nchini humo aiwa na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuwasili kwa ujumbe huo, mwenyekiti wa Baraza la Biashara nchini, Evarist Maembe alisema uzinduzi wa baraza hilo utaimarisha biashara baina ya nchi zote mbili na pia kuwaunganisha na Chama cha Wafanyabiashara wa nchi za Ghuba (Gulf Chamber).
Alisema ugeni huo ambao pia utafanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda utakuwepo nchini kwa siku kadhaa ambapo ytatembelea Zanzibar na Bagamoyo na kufanya majadiliano ya kibiashara na wadau wa sekta hiyo nchini.
“Tutajadili jinsi ya kubadilishana watalaam wa fani mbalimbali za kilimo na kuangalia mahitaji ya wenzetu hao ambao kimsingi wangependa kuagiza vyakula kutoka nchini ambao ni karibu badala ya kufanya hivyo Israel ambako pia ni mbali kulinganisha na Afrika.
Maembe alisema hadi kufikia hatua hiyo ni kutokana na ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini Oman ambayo iliwasisimua wafanyabiashara wa nchini humo ambao waliona kuna haja ya kuwa na mtandao wa ushirikiano na Tanzania ambako raia hao wa Oman wana uhusiano nako.
“Walivutiwa na ukweli kuwa tunaunganishwa na historia kwani wao wanaamini kuwa uku Tanzania hasa Zanzibar wana ndugu na jamaa zao ambao wapo huko na kikubwa zaidi ni kuwa kuna mwingilino wa tamaduni baina yetu na wao” Maembe alisema.
Alibainisha kuwa Oman wanatamani vitu vingi kutoka huku ikiwa ni pamoja na mbogamboga kama bamia, nyanya chungu na mazao mengine ambayo kwao hakuna lakini nchini yanapatikana na kikubwa zaidi wanayafahamu kutokana na mwingiliano wa kiutamaduni uliopo.
Wafanyabiashara wa Oman wakiwa katika picha ya pamoja na balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Ali Ahmed Saleh (wa tano kushoto) na mwenyekiti wa baraza la biashara Evarist Membe (wa tatu kushoto).
Baozi wa Oman nchini, Mhe. Ali Ahmed Saleh (kulia) na mwenyekiti wa baraza la biashara, Evarist Membe wakitoa maelekezo kwa wageni wao kabl;a ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere.
Mwenyekiti wa Baraza la Biashara nchini, Everist Membe akiwapokea wafanyabiashara kutoka Oman
Natoa shukrani kwa rais wetu kwa kazi nzuri anazo fanya wananchi nasi tujitahidi tusimuangushe kiongozi wetu shime wananchi.
ReplyDeleteHaya wtz deal hilo mpaka nyanya chungu ni deal sio kukaa na kufanya ujambazi kwa kisingizio hakuna kazi.
Changamkia tender hiyo ondoa ukwasi wa maisha