Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii leo wametembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa. Lengo la ziara hii ni kukagua utekelezaji wa shughuli za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika utoaji wa Mafunzo ya Maendeleo ya Jamii kupitia chuo hiki. Katika ziara hii, wajumbe wa kamati walipata fursa ya kupokea taarifa ya chuo na kutembelea maeneo / miradi mbalimbali ya chuo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (mb.) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kilichopo Wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Saidi Mtanda (Mb.) wakikagua maeneo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba na kutoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, katika baadhi ya maeneo yenye kuhitaji maboresho.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Kati) pamoja na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba, (Kulia, mwenye nguo ya kahawia) Bibi Santina Mbata wakiwapitisha Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika Majengo / miradi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wakati tunakua tulikuwa tunafuata totos hapo chuoni kutoka mji mdogo wa John's Corner Mafinga!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...