Baadhi ya dawa zinazodaiwa ni feki


TANGU kuanzishwa kwa kauli mbiu ya kilimo kwanza, kumekuwa na juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha wakulima wanaingia kwenye kilimo cha kisasa.

Juhudi hizo zimetiliwa nguvu zaidi katika kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo ili kuwafanya wakulima kuzitumia na kuimarisha kilimo chao.
Baadhi ya dawa zinazodaiwa kuwa feki

Pamoja na juhudiz hizo za serikali, bado kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wakulima juu ya pembejeo hizo za kilimo, ambapo zimekuwa zikilalamikiwa kwa kuharibu mazao.

Kwa mfano, mboleo ya Minjingu imekuwa ikilalamikiwa na wakulima kwa kile kinachoelezwa kukausha mazao yao na kutokuwa na virutubisho vya msingi kwa ajili ya ukuaji wa mazao.

Katika kuonyesha kuwa kuna matatizo ya msingi katika kupatikana kwa dawa na mbolea kwa ajili ya mazao ya wakulima, kelele nyingi zimekuwa zikisikika pia bungeni kulalamikia mbolea na dawa feki.  Katika Bunge lililopita baadhi ya wabunge waliitaka serikali kushughulikia malalamiko ya wakulima kutokana na mbolea na dawa zinazosambazwa na mawakala kutokuwa na ubora.

Wabunge hao walieleza kuwa pamoja na serikali kuhamasisha wakulima kwa kauli mbiu ya kilimo kwanza lakini kumekuwa na tatizo la mbolea na dawa hizo kutokidhi viwango na matokeo yake kuua mazao.  Katika kujibu malalamiko ya wabunge, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwahi kueleza kuwa serikali inafanyia kazi malalamiko ya dawa na mbolea ya Minjingu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hawa jamaa ni wabaya sana wameshaniuzia dawa ya kusafisha CHOO feki. Ukitaka kuwajua anza kupatana nao basi mwisho watakubali bei ndogo kabisa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...