Wanamuziki wa Bendi ya FM Academia "Wazee wa Ngwasuma" wakilishambulia jukwaa kisawasa wakati wa Onyesho la kufunga Mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014,lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge,Victoria jijini Dar es Salaam.
Wazee wa Ngwasuma wakiendelea kutoa burudani ikiwa ni sehemu ya kukonga vyema nyoyo za mashabiki wao walikuwepo kwenye Ukumbi huo.
Pacho Mwamba na Nyoshi El Sadaat wakiongoza safu ya uimbaji katika onyesho hilo.

Madansa wa FM Academia wakivuta pumzi kabla ya kuingia tena jukwaani.
Wadau wa TBC1,Chacha Maginga (kulia),Angel Msangi na wengine wengi wakiwa ni sehemu ya mashabiki lukuki wa Bendi ya FM Academia waliokuwepo kwenye Ukumbi huo,wakati wa Onyesho ya funga mwaka na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2014.
Wadau mbali mbali wakiwa wamefurika kwenye Ukumbi huo kuusherehekea Mwaka Mpya sambamba na Bendi yao pendwa ya FM Academia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...