Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, 
Mhe. Bernard K. Membe 

Na Mwandishi wetu, Addis Ababa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kuanza kesho Alhamisi tarehe 30 Januari, 2014 mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa AU uliofanyika tarehe 27 na 28 Januari, 2014 ambao Mhe. Membe aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.
Kaulimbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni “Kilimo na Usalama wa Chakula” unalenga kuweka mikakati madhubuti katika kuhakikisha kilimo kinakuwa mkombozi wa watu Barani Afrika kwa kuwainua kiuchumi na kuondokana na wasiwasi wa njaa unaolikabili Bara hili mara kwa mara.
Mkutano wa Wakuu wa nchi pia utapokea Ripoti mbalimbali ikiwemo ile ya Kamati ya Kimataifa ya Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (CAHOSCC) iliyokuwa chini ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali unatarajiwa kumalizika tarehe 31 Januari, 2013.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mi sijafurahia uamuzi huu wa Mheshimiwa Rais. Kila mwaka, nimeshazoea kumuona rais wetu akihudhuria mkutano huu. Kauli mbinu mwaka huu ni kuhusu kilimo - hoja naamini ni sekta inayopewa due importance na rais wetu.. Kama yeye hakuweza kuhudhuria, basi Dr Bilal ama mtoto wa mkulima wangeweza kum-represent. Ingeonekana wema kama tungepeleka a high powered delegation

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...