Kwa maneno yake Zitto Kabwe: "Nimeomba mahakama kuzuia kamati kuu ya chama changu kunijadili mpaka rufaa yangu isikilizwe na Baraza Kuu la chama. Sijaomba kuzuia kamati kuu kuendelea na kikao chake. 
 Nimeomba kamati isinijadili maana nina rufaa kwenda Baraza Kuu kwa jambo hilo hilo ambalo kamati kuu inataka kuliamulia. 
Wakili wa chama Tundu lissu aliweka mapingamizi akisema mahakama haina mamlaka kujadili masuala ya vyama na wanachama wao. 
 Jaji John Utumwa katupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu. 
 Mahakama ndio Chombo cha kutoa haki. 
Asante Wakili Albert Msando. Haki itatendeka…"
 Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo, ambapo aliwasilisha ombi la pingamizi la yeye kutojadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinachotarajia kufanyika kesho, hadi rufaa yake ya kupinga kuenguliwa wadhifa huo kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni Wakili wa Zitto, Albert Msando. Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kinachotarajiwa kufanyika kesho kutomjadili kwa namna yoyote
                                Zitto Kabwe akiingia mahakama Kuu Dar es Salaam leo
 Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika kupinga hoja hiyo mahakamani.
 Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama
Zitto ana wakili wake Msando wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa wakisubili uamuzi wa mahakama, ambapo Zitto aliibuka dedea kwa pingamizi lake kukubaliwa hivyo kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika kesho kukatazwa kumjadili kwa namna yoyote Zitto. Picha na Kamanda wa Matukio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. I am proud of Zitto katika nyanja zote.Chama cha Kibabe kinachoonyesha kuendeshwa kwa mawazo ya wachache taratibu ukweli wake uradhihirika na Lissu ataporomoka sasa hivi asipoenda mbali na na hao atajeopadise usomi wake.

    ReplyDelete
  2. Sijaelewa mbona Lema yupo hapo mahakamani na si wakili. Kuna nini?

    ReplyDelete
  3. It is obvious, Zitto is s traitor.. no doubt at all!

    ReplyDelete
  4. Siasa za bongo za kinafiki. hawa viongozi wa juu wa CHADEMA wanaogopa Zitto kugombea uenyekiti kwani atashinda ndio maana wanamzulia zengwe ili wamtimue uanachama kupitia hiyo kamati kuu yao. Wamepigwa chini na hatma ya Zitto itakuwa ni uamuzi wa baraza kuu. Tuseme kweli wamemtumia kujenga chama na kupata wanachama lakini wamemuwekea limit ya kutokugombea uenyekiti. Walizani mahakama kuu ni ya Swai.

    ReplyDelete
  5. Lema yeye ni bendera ametumwa na wazee wa mabavu na pia hana kazi ya kufanya kwa wananchi wa jimbo lako miaka nenda miaka rudi anazurura tu

    ReplyDelete
  6. Tundu, jieleze vizuri kwa huyo mtoto wa mwenye nyumba kwa nini umeshindwa kesi. Vinginevyo atakuchongea kwa baba yake na utatimuliwa nyumbani kwao!

    ReplyDelete
  7. Mtoa maoni namba 2, si kila anayeinekana mahakamani ni wakili. Hakuna sheria inayomzuia mtu yeyete kwenda mahakani. Mbali na mawakili, mahakamani pia utawaona mahakimu, askari polisi na magereza, wazee wa mahakama, makarari, watu wanaoshughulika na usafi, waandishi wa habari, washitaki, washitakiwa, mashahidi, forensic experts, mtu yeyote anayejisikia kwenda kusikiliza kesi tukiwemo mimi na wewe, nk. Kwahiyo mh Lema anaingia katika kundi moja kati ya hayo niliyoyataja. Umefanya vizuri kuuliza na nafikiri utakuwa umeelewa.

    ReplyDelete
  8. wewe zito nini wewe!yaani unajitumia mwenyewe massge du! kalaga baoo!!!!!!

    mdau
    mwandiga!

    ReplyDelete
  9. Chadema acheni ubabe, kama chama mnataka kuendesha kibabe, je nchi mnayotaka tuwape yenye wendawazimu na vichaa mtaiweza kweli?

    ReplyDelete
  10. Hapo ndio mwisho wake kisiasa Bw. Nyepesi

    ReplyDelete
  11. Zitto needs to grow and man up, I cannot believe he is taking on his own party. How long will this go on? Who knowns. He has to tell the truth on what actually happened. He promised to tell us about the bank accounts o/s, am still waiting, he could name those in Parliament but anaogopa nini?

    ReplyDelete
  12. Msulia na Nguvu za ajabu za Kisiasa za Zitto Kabwe ndio zinathibitisha ukomo wa Siasa za Kichagga!

    Hapa tunashuhudi Siasa za Kichagga za Chadema zinapogonga mwamba mbele za Mjanja wa mambo Zitto Kabwe!!!

    ReplyDelete
  13. Wachagga wa Chadema,

    Bila ya kumpatia Uenyekiti na yeye Zitto kuwa Mgombea Uraisi 2015 ndio tuseme Chadema imakufa rasmi!!!

    Tazameni kule Sudani Kusini jinsi Raisi Salva Kiir anavyoleta Ukabila kwenye Chama na Serikali na jinsi unavyoleta maafa.

    Hapo ndio mtathibitisha ya kuwa Chadema sio ya Wachagga kwani Zitto Kabwe kuwa Mwenyekiti ndio ninyi mtageuka kuwa mawe?

    ReplyDelete
  14. Hivi mnamtetea Zito mnajua aliyokuwa anayafanya kukihujumu chama chake? Muwe mnasoma taarifa huru mjue ukweli wa mambo msiwe kama MADODOKI jamani.

    ReplyDelete
  15. Haya Maamuzi ya Mahakama Kuu kumpa Zitto Kabwe Ushindi wa Pingamizi unazidi kumnyanyua kumpaisha na kumpa Umaarufu ktk Chama!

    WACHAGGA WA CHADEMA lazima muukubali ukweli unao wauma sana ya kuwa sasa Zitto Kabwe hashikiki, anazidi kupaa na kuzoa idadi kubwa ya wafuasi huku ninyi Wabaguzi wachache mnaombana mkionekana kibindoni mna agenda ya siri.

    Mnavyo mpaisha wenyewe kisiasa mtambeba vipi Zitto Kabwe?

    1.Dr.Slaa Padri Mstaafu amegombea Uraisi mara zaidi ya 2 amepigwa chini akapata Kura sawa na namba za viatu ktk asilimia.

    2.Mwenyekiti wenu Mjanja wa Mjini Freeman Mbowe amegombea Uraisi mara zaidi ya 2 naye ameanguka vibaya sana, hadi akaanza uchochezi ikapelekea akabebwa na Helikopta hadi Arusha na kufikishwa Mahakamani!

    Hakuna jinsi ni lazima Wachagga muukubali ukweli utakao wauma saaana ya kuwa huu ni wakati wa Jogoo wa Chadema Zitto Kabwe kuwa Mwenyekiti wa Chama na pia Mgombea Uraisi 2015!!!

    ReplyDelete
  16. Zitto Kabwe DUMEEE !!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. Ohhh Mwenyekkiti Mpya na Mgombea Uraisi Chadema 2015 huyooo Zitto Kabwe!

    Wachagga mmesha funikwa Kisiasa kilicho baki mkauze supu kwenye mabaa na kusafisha Shoe shine za viatu.

    ReplyDelete
  18. Mimi nafikiri hata Padre Slaa ni kivuli tu.Bali wazee wenyewe wametulia huko moshi na kutoa Amri tu. Nafikiri padre amkabidhi cheo muumini mwenzie mchungaji msigwa kukiendeleza chama zaidi.

    ReplyDelete
  19. zzk ni mzalendo sana ss wana shy tuna mtakia kaz njema ktka safari yake kama ya lowassa,lisu haufai kabsa zzk kakukosea nini muulize mwezako kilicho mtokea hana mkono mpaka leo;by ngogombeda,magu mwanza. zzk mungu ataksaidia tu.

    ReplyDelete
  20. Mimi naona watu wengi mna wivu sana na wachagga labda kwa sababu wamewazidi kwa kila kitu.
    Ukweli utabaki kwamba ZITO KABWE ni kirusi ndani ya CHADEMA.

    ReplyDelete
  21. Acheni Dhambi ya Ukabila. Mwl. Nyerere alisema dhambi ya UBAGUZI haiishi. leo mnasema Wachaga kesho mtasema WAHA, keshokutwa sijui itakuwa kabila gani. Na kwa kwa taarifa ya hao WABAGUZI wa ukabila. Mwanasheria wa Zitto Bwn. Alberto Msando naye ni wa KILIMANJARO sasa naye ni MKABILA?

    NAwasilisha.

    ReplyDelete
  22. Mbowe akigombea tena uenyekiti CDM ntaconclude kuwa ni mbinafsi, mroho wa madaraka na mkabila pia.. Na ntaelewa kwanini anampiga vita ZZK

    ReplyDelete
  23. wametuzidi ndio maana hatutaki waongoze nchi wataona wananchi wote ni sawa na wao! hata baba wa taifa aliliona hilo.

    ReplyDelete
  24. Ninyi mnaotoa maoni hapa mbona kama vile mnatumia lugha ya chama kingine na si chadema? na mbona mnashabikia zaidi mtu na si taratibu, kanuni na katiba ya chadema? mbona kama vile mmeshikwa na mtanziko kuhusu yanayomkuta Zitto? mbona kama vile mnachanganyikiwa mnaposikia Zitto anafukuzwa uanachama? haya mimi napita tu. kilalakheri buriani ccm.

    ReplyDelete
  25. Mtani wangu zito kabwe oyeeeeeeeeee, pasua anga dogo, hawakuwezi kabisa, kwanza wakuache uthubutu, waone, ikulu nje nje 15, wakiogombea mbowe na bunduki, hawapati kitu, sisi watanzania tunayo macho, tunaona vema, hatuwezi kumweka mtu mwenye mitusi, mizengwe, kashfa kwa wenzake, lakini wewe umetulia, ukitoa hoja ni ya nguvu na nzito, unaweza sana mtani, ila sasa oa mapema mtani, 15 ikulu ya kwako kabisa iko wazi. waache waangaike wachaga, mtani wako jita girl from mara.

    ReplyDelete
  26. wana wasiwasi hao, hebu wapime pressure zao, nadhani roho zinawauma sana, kiongozi mzuri ni yule anayekubalika na watu, utashi wake, mwonekano wake, usikivu, kauli zake, weledi wa kuelewa mambo, uzungumzaji anapokuwa kwenye kadamnasi, hebu mwangalie ZZK anapowasilisha hoja bungeni, anakuwa ametulia kwa uhakika. pia muangalie mbowe loooo! kama anagombana vile, sijui uasili wa kule kwa wagechaji (kanda maalum) yumo nini kule kwetu mura mura. haaaaa, ZITO KABWEE PAMBANA MPAKA KIELEWEKE MDOGO WANGU. TUNAHITAJI MARAIS VIJANA. Zito oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  27. ZITO usihofu kufukuzwa wewe unaweza,na najua hata wakikufukuza simama mwenyewe 2015.Bigup ibara ya 125(1)(c)ya katiba mpya kama itapitishwa.Hii itawaokoa watu walionyimwa haki kama zito kusimama wenyewe kama wagombea binafsi.

    ReplyDelete
  28. HE HEH EEH! Wanafikiri walivyomnyamazisha wangwe wamefunga kazi looh! mambo ndio kwanza aah! kwa zito watasota sana wengi tumeona kuna chama na vyama ngoma 15 hiyo cha mtoto mambo ya kutawaliwa na ukoo mmoja marufuku baba mkwe, mkwe, mamammkwe, kaka, shemeji wao wale tu wengine wasote barabarani hata mwalim alikataa aaah yangu macho sina chama chochote yetu macho ila zzk wakaze wasikuzoee kama unga wa udaga

    ReplyDelete
  29. The mdudu,,anasema jamani ndugu zangu busara itumike kwenye kasheshe kama hiyo ZZK amekipaisha sn Chadema hilo lazima tulikubali sote kama watanzania ila kama busara haitakuwepo na huyo ndugu ZZK akafukuzwa,,basi kitakachotokea ni hiki,,zzk atachukua uwamuzi wa kuzunguka mikoa yote na kuchukua wanachama lukuki toka Chadema na CCM pia coz huyo kijana anamvuto sn kwenye jamii ya watanzania,,na mfananisha na mvuto wa Afande Sele kwa wana Moro

    ReplyDelete
  30. Zito pambana nao hao , wamesahau sasa mpaka sasa WANATAKA WASITAWALIKE MPAKA KWENYE CHAMA CHAO MAANA WALISEMA NCHI HAITATAWALIKA. hakuna wa kuwapa kura hao nani anapenda watu wasio wazalendo hawapendi amani na kila kukicha kutaka mapambano , kama wanataka mapambano waende SUDANI KUSINI.

    ReplyDelete
  31. acheni unafiki nyie vibaraka wa mafisadi, dr slaa lazima awe rais wa nchi hii hata wanajeshi wanamkubali, nyie mnayesema ni nani, nchi hii bila dr slaa atutafika mwisho, na kwa taarifa yenu mafisadi wajiandae, dr slaa urais wako hilo linajulikana wazi, wala msisumbue akiri zenu huyo babu ndio rais 2015 kama mnabisha mtaona 2015.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...