Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa (kulia) mara baada ya kuwasili katika ofisi za makao makuu ya mkoa wa Mara.
 Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Patrick Kasera akifafanua kwa wafanyabiashara wa mkoani Mara juu ya mashine za EFDs na kusema kuwa mashine hizo kazi yake kuu ni kutunza kumbukumbu za biashara hasa manunuzi na uuzaji na sio mfumo wa kodi kama ilivyopokelewa mwanzoni na wafanyabiashara nchini.
 Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akiongea na wa wafanyabiashara wa mkoa wa Mara juu ya umuhimu wa utumiaji wa mashine za kodi za kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara hao kukusanya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ili Serikali iweze kutoa mahitaji ya kijamii na uchumi kwa wakati.
 Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo pichani) alipokuwa alipozungumza na wafanyabiashara hao jana mjini Musoma katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo.
 Baadhi wa wajumbe waliohudhuria kikao cha wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipozungumza nao ili kuwaelimisha juu ya masuala mbalimbali ikiwemo mashine za EFD wakati wa ziara yake ya kikazi mikoa ya kanda ya Ziwa.
Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza  Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa alipozungumza na wafanyabiashara hao jana mjini Musoma katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo wakati wa ziara yake ya kikazi mikoa ya kanda ya Ziwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Umetubania tusitoe maoni kwenye msimamo wa ligi. Nyekundu, inamaana hata kama wanashinda hawasogei juu?

    sesophy

    ReplyDelete
  2. Muraaa, amang'ana !!!

    Nitoe Kodi ya nini kwa EFD wakati Braza wangu Profesa Sospeter Muhongo yuko Wizara ya Madini na Umeme?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...