Ankle habari. Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana na na ajali  mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Mdau Sixmund

 Hakuna cha kufanyika kutokana na moto mkubwa na moshi mwingi wakati magari hayo yakiteketea
 Mlipuko mkubwa wakati matenki ya mafuta yakilipuka
Askari wa kikosi cha zimamoto wakijaribu kuuzima moto huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mimi nimeshuhudia hili tukio kwa macho yangu na wakati linatokea mi nilikuwa narudi dar kiukweli si mtu mmoja aliyeteketea, wakati ajali inatokea nilikuwa peke yangu ambaye nateremke kilima kutokea mizani ya mikese hakukuwa na gari nyingine nyuma yangu, ghafla niliona hilo lorilinahangaika kwa kufail break nilichokifanya nikasimama na kuanza kurudisha gari yangu nyuma, ghafla moto ukaanza kuwaka maeneo ya kwenye betri na baada ya muda kidogo ukashika kwenye eneo la nyuma ya hilo lori, kiukweli nilitetemeka sana mana haikuchukua dakika 5 moto ukawa mkubwa sana, tukawa tunajiuliza na wanakijiji wa pale je kuna mtu atakuwa ametoka? wakati tunajiuliza kidogo tukaona mtu anatoka kwenye lile lori linalowaka anatambaa kwa magoti kama mtoto na alikuwa amechoka sana na kuumia ilibidi kijana mmoja ajitoe muhanga kumuwahi na kumnyanyua na ndipo wengine tukasogea kumbeba pongezi sana kwa yule kijana alivaa tshirt ya njano na suruali nyeusi mana kwa mlipuko na vishindo vilivyokuwa vinatokea pale ilikuwa ni kama mabomu ya mbagala, tulimuuliza yule jamaa akasema kwenye gari lao walikuwa wa nne hivyo wenzake watatu hawakufanikiwa kutoka, nimechukua picha ambazo zipo very clear nitakutumi michuzi.
    Mdau

    ReplyDelete
  2. Wazima moto wa mafuta kwa maji!!! Ha ha ha! Kweli kuna maajabu hapa kwetu! Maskini wazima moto wetu!!!

    ReplyDelete
  3. Bado kuna vijana wenye imani na ubinadamu.

    Hongera sana kijana kwa kumsaidia mwenzako wakati wa shida kama hii. Mwenyezi Mungu atakupa kheri nyingi sana.

    Na vijana wengine waige mfano wake na siyo kukimbilia ngawira tu wakati wa ajali.

    ReplyDelete
  4. Tupe tuone maana camera haijui kudanganya !

    ReplyDelete
  5. Mdau wa pili hapo juu,kuwa hodari wa kupima mambo.Hapo mafuta yalikuwa yote yameshaungua ,kinachozimwa hapo ni matairi na chagaa chagaa zilizobakia tuu.

    ReplyDelete
  6. Heh,heh waandashi jamani.Andikeni kwa uhakika.mwatwambia magari mawili yamegongana uso kwa uso.Aliyeishudia anasema moja tuuu kwanini mdanganye.Asante mdau shuhuda.I appreciate your first hand information.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana wote waliopata ajali mbaya sana hii. Yaani pia hapo mazingira yanachafuliwa kwa huo moshi ambapo sijui yalikuwa mafuta gani! Cancer zitaisha au kuongezeka? Obvious risk za cancer kuongezeka ni kubwa sana. Hewa hiyo imebeba particles zinazodhuru mwili wa binadamu, particles hizo hukaa hewani kwa muda mrefu hata miaka! Mungu iponye Tz na watu wake.

    ReplyDelete
  8. Mpaka lini madereva watakuwa makini kuendesha magari? kila siku ajali tanzania jamani. Mimi sielewi utaratibu gani uchukuliwe ili kuepusha ajali hizo. Poleni sana wafiwa wa ajali hiyo

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli haya magari hayaruhusiwi kubeba abiria, ila ndio kibongo kibongo yanabeba. Poleni wafiwa.
    Halafu unakuta maeneo ya ubungo Kuna vijana wanafungua koki za matenki Na kuiba mafita Nalo pia Ni janga lengine ambalo ipo siku laweza kuleta madhara hasa ukizingatia foleni za ubungo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...