


Pili, tunatambua mchango wa Serikali katika kuhamasisha uundwaji wa Jumuiya za Watanzania nje ya nchi kama njia bora ya kuwaunganisha Watanzania kujadili mambo muhimu kwa nchi yao na maslahi yao. Jumuiya hizi zinaundwa na Watanzania na Watu wenye asili ya Tanzania na marafiki wa Tanzania.
Watanzania wanaounda jumuiya hizi wamekuwa ni mabalozi wazuri katika kuitangaza Tanzania nje ya nchi na vile vile wana mchango mkubwa wa kuendeleza utamaduni wa Mtanzania nchi za nje, lakini vile vile kudumisha huduma za biashara na kubadilishana utaalamu kati ya Tanzania na nchi nyingine kupitia programu mbalimbali kama za mawasiliano ya kijamii, michezo na mambo mengine mengi.
Kihistoria Watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi wamekuwa wakishiriki katika mambo ya kimaendeleo na wamekuwa na sifa nzuri katika mahusiano yao na nchi nyingine na katika kudumisha lugha ya Kiswahili, utalii, mahusiano ya kibiashara na viwanda kati ya Tanzania na nchi nyingine na bila kusahau elimu katika fani mbalimbali.
Tatu, tunatambua mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kuwasilisha maoni ya wana-diaspora kwa Tume ya Katiba ili yafikiriwe na kuwekwa ndani ya Katiba Mpya.
Na ni matumaini yetu kuwa wizara hii na taasisi nyingine husika zitashirikiana nasi katika kuhakikisha kuwa suala la uraia pacha linawekwa kwenye Katiba mpya ya Tanzania. Tunazidi kuiomba serikali ma wizara zake kuhakikisha kuwa changamoto zetu na suluhisho zake zinaingizwa kwenye katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiwemo vile vile suala la uraia pacha.
Nne, mchango wetu kama Watanzania wanaoishi kwenye diaspora ni mkubwa sana katika kuendeleza uchumi wa Tanzania.
Kwa mfano, mwaka wa 2012 Watanzania waishio nje ya nchi walituma pesa kiasi cha dola milioni 250 kwenda Tanzania. Idadi ya Watanzania waishio nje ya nchi wanakisiwa kuwa asilimia 5 ya Watanzania wote, yaani karibia watu milioni 2.25 (Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje). Na kiasi cha fedha zinazotumwa Tanzania kutoka kwenye diaspora kinazidi kuongezeka siku hadi siku. Hivyo sisi wanadiaspora bado tunachangia sana katika shughuli za maendeleo ya nchi yetu.
Tukija kwenye vyama vya siasa, sisi Watanzania tunaoishi ughaibuni tunaviomba vyama vya siasa vyote vya Tanzania kwa pamoja bila kujali itikadi zao kulipigia kura suala la uraia pacha ili liingizwe kwenye katiba mpya.
Sisi kama Watanzania wa ughaibuni lengo letu ni kujenga umoja baina ya Watanzania na kuitangaza nchi yetu nchi za nje na hasa tunapoishi ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano mazuri kati yetu na nchi zilizotukaribisha uhusiano ambao unavuka mipaka yetu na kuifanya Tanzania kuwa na mahusiano mazuri na nchi nyingine.
Tunaomba vyama vyote vya siasa vikubali maombi yetu ya kuwa na uraia pacha, kupewa haki ya kupiga kura “voting right” na kepewa haki ya kurudi Tanzania “right of return” ikiwa ni pamoja na sisi tupate wawakilishi wetu kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano na Serikalini ili tuweze kwakilisha changamoto zetu na tuweze kuijenga Tanzania pamoja na watanzania wengine.
Tukija kwenye Bunge Maalumu la Katiba, kwanza kabisa tunawapongeza wawakilishi wote wa Bunge Maalumu la Katiba kwa kuteuliwa kwao na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kushiriki katika Bunge hilo muhimu litakalotuletea katiba mpya.
Pili tunapenda kumpongeza aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Bunge hilo. Tunawaomba wawakilishi wote wa Bunge Maalumu la Katiba kumpa ushirikiano Mwakilishi wetu kutoka Diaspora Mheshimiwa Kadari Sanga ili pale atakapoziwakilisha changamoto zetu zipatiwe suluhisho zuri na la kudumu.
Tunawaomba wabunge wote walipigie kura ya ndio suala la uraia pacha ili liingizwe kwenye katiba maana lugha ya sasa iliyotumika kwenye rasimu ya katiba bado haisema wazi kama uraia pacha unaruhusiwa. Tunaomba katiba iseme wazi ni ruksa kwa Mtanzania kupewa uraia pacha.
Mwisho tunawashukuru Watanzania wote kwa kuielewa hoja hii.
Tunawaomba wasaini petition yetu tuliyoiweka kwenye blogi mbalimbali ili watusaidie katika kutimiza lengo letu la kupeleka sahihi za Watanzania kwa wahusika wa suala hili. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika.
Imeandaliwa na Deogratius Mhella,
Katibu wa vikao vya Jumuiya za Watanzania Marekani na DICOTA,
katika jitihada za Watanzania kuelimisha umma juu ya maombi yao ya uraia pacha.
Ubishoo tu, hamna lolote zaidi ya kutaka kuringishia hizo passport zenu 'zilizopinda-pinda'.
ReplyDeleteKwani mlivyochukua uraia wa nchi nyingine hamkujua kwamba Tanzania hairuhusiwi?
Na nyie wenye ndoto za urais, hao Diaspora nao mtawakatia tiketi za ndege waje kupiga kura za maoni kwenye vikao vya chama?
CCM, Chadema ... hivi hamuwezi kuchangia maendeleo ya nchi yenu hadi mjiingize kwenye siasa?
Kwanza sio kweli kwamba wote tulio nje tunataka uraia pacha, ebu wizara na jumuiya (kama bado zipo manake Uingereza haipo tena), toeni data za ukweli.
Sisi watanzania tulioko bongo tunasema - Mshika kuwili hukosa kote, amtumikiae mabwana wawili hukosa kote. Sasa nyie mnatii taifa gani na je kukiwa na ugomvi kati ya tanzania na uko mliko kuwa na uraia je mtakuwa adui wa nani? BASI SISI RAIA WA TZ HATUTAKI. Alex bura dar
ReplyDeleteKufuatia comments za baadhi ya watu katika blogs tofauti kuhusiana na hoja hii ya Uraia pacha imenionyesha kwa kiasi gani uelewa wa baadhi ya Watanzania kuwa ni mdogo na vilevile baadhi yao kuwa waropokaji hata bila kuwa na hoja za kimsingi.ie wachangia 1&2 above.Hivyo ushauri wangu kwa wana Diaspora ni kuepuka kujiingiza ktk mijadala na watu kama hao kwani hoja ya Dual citizenship haiwezi kuamuliwa na watu wenye uelewa mdogo kama hawa.
ReplyDeleteHoja hii ni nzito na muhimu sana katika Taifa letu kwa wakati huu na ningependa tujenge hoja kwa watu wenye uwelewa ili Waheshiwa waweze kutoa maamuzi for the interest of the Nation.Dont west your valuable time kuingia kwenye mijadala isiyokuwa na tija.
WA 9/11 walikuwa na uraia WA pasipoti mbili tafakariii
DeleteMimi nilikuwa sielewi umaana wa Uraia wa nchi mbili. Sasa naanza kuelewa. Na nadhani hawa ndugu zetu wanatufumbua macho. Endeleeni kutuelewesha Faida za Uraia pacha ili tuutetee. Mpaka sasa sioni tatizo kama Watanzania wataruhusiwa kuwa na Uraia wa nchi mbili.
ReplyDeleteMshika mawili moja humpokonya...chagua kusuka au kunyoa huwezi kufanya vyote. Hakuna Uraia pacha labda waweke ukazi wa kudumu (permanent resident) sio uraia.
ReplyDeleteWe mchangiaji wa mwisho mbulula kweli, km mmeshachagua nchi nyingine kuwa yenu huku si hakufai mnapatakia nini sasa, eti watanzania tuna upeo mdogo sawa nyie sio watanzania ndio maana mnaupeo mkubwa bakini huko huko au jibadilisheni muwe wazungu nyie ndo wale mnaodai bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko binadam Tanzania sasa mnatumwa km mbwa huko mnatamani kuwa binadam, kaeni hukohuko manyang'au nyie
ReplyDeleteMlisha ukana Utanzania kazi kwenu!
ReplyDeleteMsimamo wetu ni PASIPOTI MOJA kwa MTU MMOJA na sio PASIPOTI MBILI KWA MTU MMOJA hiyo hapana!
Sasa ndugu zetu tutawaamini vipi haswa katika masuala ya Uongozi na Usimamizi wa mambo?
Mfano wewe mwenye Pasipoti 2 tukupe Madaraka ya kusimamia Shirika moja ukahamisha FEDHA ZOTE kutoka huku Tanzania halafu ukakimbilia kwenye PASIPOTI YAKO INGINE je tutakupata vipi?
Je nchi yao ya Pasipoti ya pili itatupa ushirikiano kukurudisha Tanzania kusimama kwenye Sheria?
Kwanza tunataka kuirudisha Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo kata kata haikubaliani na masuala kama hayo ya PASIPOTI MBILI KWA MTU MMOJA!
Wadau Madiaspora:
ReplyDeleteKama mnataka Utanzania sawa tutawapa na pia Uraia pacha kwa mashariti haya hapa chini:
1.Kwa kuwa wengi mlisha ukana Utanzania, mtahitaji kwenda Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sharia miezi 6 na kula Kiapo cha Utii kwa nchi yenu tena.
2.Kwa kuwa Siasa ya Ujamaa bado vionjo vyake tungali navyo kama Mdau mmoja alivyogusia jana, mtawajibika kuwa na Mashamba angalau ya mfano vijijini Tanzania hata kama mtakuwa mmeajiriwa na kuwa Wakurugenzi Mijini Tanzania mtakapo rudi nchini.
3.Mtawajibika kukubaliana na Msimamo ya kuwa mtaruhusiwa na kushiriki Upigaji wa Kura na Siasa, lakini ngazi yenu ya juu ktk Uongozi ni Ujumbe wa Serikali za Mitaa na Udiwani.
Je, mtakubaliana na Mashariti hayo?
kama huna passport ya Tanzania ww si mtanzania.tusipotezeane muda.
ReplyDeleteAnonymous 3 naona lugha gongana (west / waste) ingawa unaona wachangiaji 1 & 2 wana uelewa mdogo.
ReplyDeleteLakini badala ya ubabe, ungetoa hoja badala ya kusisitiza matabaka ya uraia pacha.
Hivi kweli tulio ughaibuni hatuoni huruma kiasi cha kujivika magwanda, kukatiwa tiketi na kwenda Dodoma?
Kwanini badala ya kupigania maendeleo ya nchi kama tunavyoona wenzetu wanavyojali wananchi wao, tunawaza kujichomeka-chomeka tu?
Naungana namchangiaji aliyesema inabidi kuwepo na kikomo cha madaraka, mwisho ukatibu kata tu.
Kwanza hata hizo passport zenyewe tayari 'tumechakachua'.
Ebu tufufue na kuimarisha jumuiya zetu zilizopo ughaibuni badala ya CCM-UK na Chadema-UK.
Tanzania Oyeee? Uraia wa nchi zaidi ya moja oyeee. Nimemaliza sina mengi.
ReplyDeleteWadau hoja hii nzuri sana. Uraia wa namna una una manufaa vile vile tusiangalie tu wale wanaojitokeza hapa na kuponda bila vigezo maalumu.
ReplyDeletehata Serikali inaungai mkono uraia wa nchi mbili tatizo lipo wapi?
ReplyDeleteMbulula acheni longolongo; tumepunguza idadi ya wazululaji bongo; tuna mjengo na rasilimali kibao bongo; kaka MICHUZI uraia wako utautema???
ReplyDelete