Mheshimiwa Balozi alifanya ziara ya kikazi wiki iliyopita huko jijini Aberdeen,Scotland kufuatia mwaliko wa Kampuni ya Afro-invest kwa ushirikiano na Scottish Development International (SDI) na Aberdeen & Grampian Chamber of Commerce (AGCOC).

Lengo la ziara hii lilikuwa ni kwanza, kukutanishwa na Ujumbe wa kibiashara unaotarajia kuzitembelea nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania mwanzoni mwa mwezi wa Febrauri. Pili, ni kujionea shughuli za SDI na AGCOC katika uratibu na uendeshaji wa shughuli za Makampuni ya kibiashara.

Kwa kuwa mji wa Aberdeen ni mahsusi kwa shughuli za mafuta na gesi, ziara hii ilikuwa muhimu sana kujifunza mengi kuhusiana na uendeshaji wa shughuli mbalimbali zinazohusiana na sekta hii.

Hata hivyo moja ya mapendekezo muhimu aliyayotoa Mheshimiwa Balozi kwa wenyeji wetu, ni kuisaidia Tanzania ijijengee uwezo ili iweze kunufaika na rasilimali zake hasa katika sekta mpya ya mafuta na gesi, ambayo hatuna uzoefu nayo.

Njia za uwezeshaji ni kwa Makampuni ya kigeni hasa yatoayo huduma kwenye sekta hii, kuingia ubia na Makampuni ya Tanzania. Njia ya pili ni kwa Makampuni au Taasisi za Mafunzo za Scotland kuandaa programme mahsusi zinazoendana na hali na mazingira ya nchi yetu ambayo ndio kwanza imegundua raslimali hii ya mafuta na gesi.

Pamoja na hayo, wenyeji nao wameishauri Tanzania kuonyesha nia ya dhati ya ushirikiano na Uongozi wa jiji la Aberdeen kwa kufanya ziara na mawasiliano ya mara kwa mara. Lakini muhimu zaidi katika hili wangependa kuona Ujumbe wa kibiashara kutoka Tanzania ukitembelea Aberdeen.

Katika ziara hii, Balozi Kallaghe alifuatana na Mkuu wa Kituo cha Biashara Ndugu Yusuf Kashangwa
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, akiongea na baadhi ya Wafanyabiashara, watakao fanya ziara ya Kibiashara nchini Tanzania baadae mwezi huu.
baadhi ya Wajumbe wa Wafanyabiashara, mjini Aberdeen, Scotland, wakijaliana jambo katika mkutano wao na Mhe. Balozi Peter Kallaghe.
Mheshimiwa Balozi Kallaghe, akimsikiliza mkuu wa Kampuni ya Afro-Invest, Bwana Desire Katihabwa, akitoa maelezo ya Kampuni yake na jinsi inavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kutangaza fursa za Uwekezaji. Wengine pichani ni Dilip Navapurka (pili kushoto) wa Kampuni ya Safarihub na mama Sheila Ritchie, Mwanasheria kutoka Kampuni ya Grantsmith, wakimsikiliza.
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, kwenye picha ya Pamoja na baadhi ya Wawakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Aberdeen, Kutoka kulia, Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa, Alec Carstairs (Aberdeen & Grampian Chamber of Commerce - President), Dilip Navapurka (tatu kushoto), Julien Masse (Aberdeen & Grampian Chamber of Commerce) na Bwana Smart Masoni, mwakilishi kutoka Kampuni ya Scotish Development International).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Michuzi kaka naomba nisaidie kuuliz atena wadau ni kadi gani ya simu naweza kutumia nikiwa marekani kupiga Bongo???? Du nitashukuru sana bro!
    Tuko pamoja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...