Mheshimiwa Balozi alifanya ziara ya kikazi wiki iliyopita huko jijini
Aberdeen,Scotland kufuatia mwaliko wa Kampuni ya Afro-invest kwa
ushirikiano na Scottish Development International (SDI) na Aberdeen &
Grampian Chamber of Commerce (AGCOC).
Lengo la ziara hii lilikuwa ni kwanza, kukutanishwa na Ujumbe wa
kibiashara unaotarajia kuzitembelea nchi za Afrika Mashariki ikiwemo
Tanzania mwanzoni mwa mwezi wa Febrauri. Pili, ni kujionea shughuli za
SDI na AGCOC katika uratibu na uendeshaji wa shughuli za Makampuni
ya kibiashara.
Kwa kuwa mji wa Aberdeen ni mahsusi kwa shughuli za mafuta na gesi,
ziara hii ilikuwa muhimu sana kujifunza mengi kuhusiana na uendeshaji wa
shughuli mbalimbali zinazohusiana na sekta hii.
Hata hivyo moja ya mapendekezo muhimu aliyayotoa Mheshimiwa Balozi
kwa wenyeji wetu, ni kuisaidia Tanzania ijijengee uwezo ili iweze kunufaika
na rasilimali zake hasa katika sekta mpya ya mafuta na gesi, ambayo
hatuna uzoefu nayo.
Njia za uwezeshaji ni kwa Makampuni ya kigeni hasa yatoayo huduma
kwenye sekta hii, kuingia ubia na Makampuni ya Tanzania. Njia ya pili ni
kwa Makampuni au Taasisi za Mafunzo za Scotland kuandaa programme
mahsusi zinazoendana na hali na mazingira ya nchi yetu ambayo ndio
kwanza imegundua raslimali hii ya mafuta na gesi.
Pamoja na hayo, wenyeji nao wameishauri Tanzania kuonyesha nia ya
dhati ya ushirikiano na Uongozi wa jiji la Aberdeen kwa kufanya ziara
na mawasiliano ya mara kwa mara. Lakini muhimu zaidi katika hili
wangependa kuona Ujumbe wa kibiashara kutoka Tanzania ukitembelea
Aberdeen.
Katika ziara hii, Balozi Kallaghe alifuatana na Mkuu wa Kituo cha Biashara
Ndugu Yusuf Kashangwa
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, akiongea na baadhi ya Wafanyabiashara, watakao fanya ziara ya Kibiashara nchini Tanzania baadae mwezi huu.
baadhi ya Wajumbe wa Wafanyabiashara, mjini Aberdeen, Scotland, wakijaliana jambo katika mkutano wao na Mhe. Balozi Peter Kallaghe.
Mheshimiwa Balozi Kallaghe, akimsikiliza mkuu wa Kampuni ya Afro-Invest, Bwana Desire Katihabwa, akitoa maelezo ya Kampuni yake na jinsi inavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kutangaza fursa za Uwekezaji. Wengine pichani ni Dilip Navapurka (pili kushoto) wa Kampuni ya Safarihub na mama Sheila Ritchie, Mwanasheria kutoka Kampuni ya Grantsmith, wakimsikiliza.
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe, kwenye picha ya Pamoja na baadhi ya Wawakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Aberdeen, Kutoka kulia, Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa, Alec Carstairs (Aberdeen & Grampian Chamber of Commerce - President), Dilip Navapurka (tatu kushoto), Julien Masse (Aberdeen & Grampian Chamber of Commerce) na Bwana Smart Masoni, mwakilishi kutoka Kampuni ya Scotish Development International).
Michuzi kaka naomba nisaidie kuuliz atena wadau ni kadi gani ya simu naweza kutumia nikiwa marekani kupiga Bongo???? Du nitashukuru sana bro!
ReplyDeleteTuko pamoja