Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpogolo amezitaka kamati zinazosimamia maendeleo ya kilimo na elimu ngazi ya kata kuhakikisha zinatimiza majukumu yake.

Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo mjini Chato wakati akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Amesema kuundwa kwa kamati za Kilimo na Elimu katika ngazi ya kata zinatoa fursa kwa wanakamati hao kusimamia masuala yote muhimu yanayohusiana na Kilimo na Elimu kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kata.

Amewataka wajumbe wa kamati kuu ya CCM wilayani hapa wanaotoka kwenye kata husika kuzisimamia na kufuatilia utendaji kazi wa kamati hizo ambazo zanaongozwa na waheshimiwa madiwani wa kata ili matunda yake yaweze kuonekana.

Amesema kamati hizo zina kazi kuu tatu ambazo ni kusimamia masuala ya kilimo na elimu katika kata husika, kuhakikisha masuala muhimu yanayohusu elimu na kilimo ngazi ya kata yanaboreshwa na kusimamia wataalamu wa kilimo na elimu ngazi ya kata.

Mkuu wa Wilaya amesema katika kipindi hiki ambapo wanafunzi waliofaulu na kutakiwa kijiunga kidato cha kwanza hawajajiunga hivyo ameziagiza kamati hizo kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti na kuanza masomo kabla ya muda wa kuripoti kwa hiari haujamalizika.

Mwaka jana Wilaya ya Chato iliunda kamati mbili za kusimamia Elimu na Kilimo ngazi ya kata mwenyekiti wa kamati hiyo ni Diwani wa kata husika na katibu wa kamati ya Elimu ni Mratibu wa Elimu kata na upande wa Kilimo ni Afisa Ugani kata.

Mkuu wa Wilaya ya Chato amesema kupitia kamati hizo ana imani kubwa Elimu na Kilimo Wilayani Chato Vitaimalika na hivyo kuondoa umasikini.

Katika kikao hicho cha kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Julai hadi Desemba Mkuu wa Wilaya aliwasilisha taarifa hiyo na wajumbe wa Halmashauri kuu CCM walihoji miradi mingi ya maendeleo ngazi za vijiji na kata kutokukamilika kwa wakati na baadhi ya miundombinu vijijini kutokukamilika kwa wakati ambapo wataalamu wa Halamshauri walitoa ufafanuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...