Waombaji 27 kati ya 28 wamerejesha fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.

Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ilikuwa leo Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.

Waliorejesha kwa nafasi ya ujumbe ni Aron Benedict Mpanduka, Elizabeth Rashid Mayemba, Emmanuel Augustino Muga, Hassan Maulid Bumbuli, Ibrahim Mkomwa Bakari, Masau Kuliga Bwire, Mbozi Ernest Katala, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa, Salum Amiri Jaba, Tullo Stephen Chambo na Urick Chacha Maginga.

Mhazini Msaidizi ni Elius John Kambili, Zena Suleiman Chande wakati Mhazini Mkuu ni Shija Richard Shija na Mohamed Salim Mkangara.

Katibu Msaidizi ni Alfred Lucas Mapunda, Grace Aloyce Hoka na Patarick Raymond Nyembera. Katibu Mkuu ni Amir Ally Mhando pekee.

Waombaji nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Egbert Emmanuel Mkoko, Maulid Baraka Kitenge na Mohamed Omary Masenga. Waliojitosa kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni George John Ishabairu, Juma Abbas Pinto.

Ni Shaffih Kajuna Dauda pekee ambaye hakurejesha fomu. Dauda alichukua fomu ya kuwania uenyekiti.

Boniface Wambura
MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI TASWA
Februari 27, 2014

Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...