Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia vifaa mbali mbali katika chuo cha mafunzo ya Amali kichofundisha wanawake pekee kutoka nchi mbali mbali Duniani ikiwemo Zanzibar,katika cha Tilonia,Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan akiwa katika siku ya pili ya ziara yake Nchni India pamoja na Ujumbe aliofuatana nao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea zawadi mara alipowasili katika Chuo cha Mafunzo ya Amali kiitwacho Tilonia,Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan akiwa katika siku ya pili ya ziara yake Nchni India pamoja na Ujumbe aliofuatana nao
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim (kulia) kwa niaba ta Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitiliana saini makubaliano ya Uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake na Chuo cha Barefoot cha India ambapo muanzilishi wa Chuo hicho Bw.Bunker Roy alitia saini (kulia) saini hiyo ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara rasmi Nchini India na ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Bw.Bunker Roy Muanzilishi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake katika Kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan pamoja na Balozi wa India Nchini Tanzania Debnath Shaw (kulia) baada ya Saini ya makubaliano ya uannzishwaji wa Chuo kama hicho Zanzibar.
Picha ya pamoja baada ya ziara hiyo. Picha zote na Ramadhan Othamn,Ikulu Zanzibar
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...