Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi(LPC) Inatoa Pongezi kwa ACP
Renatha Mzinga(pichani) aliekuwa Ofisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Lindi kwa kuteuliwa na MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu kuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa LINDI.
Taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari
Mkoa wa Lindi,Abdulaziz Ahmeid ameeleza kuwa kuwa Klabu hiyo Imepokea
mabadiliko hayo na kuhaidi Ushirikiano mkubwa baina ya klabu na Jeshi
hilo.
"Kwa niaba ya wanahabari nampongeza Mkuu wa Jeshi hilo IGP Mangu kwa
uteuzi huu nasi tutamuunga mkono katika kazi zetu za kila siku kwa
kuwa kwa kipindi kifupi alichokuwapo Lindi Tumeona Ushirikiano wake
kwa wanahabari kwa kujadiliana na kuwa huru kutoa habari Isitoshe
tumeshuhudia alivyoweza kuwaunganisha Polisi na kujua baadhi ya
Changamoto zao hususan Alivyowaunganisha askari wa kike(WP) Katika
kuunda mtandao wa polisi wanawake hali iliyoonekana ni mabadiliko
makubwa'
Hivi karibuni Kamanda Renatha alifanikisha zoezi la Usafi na kutoa
misaada kwa kituo cha walemavu kilichopo Manispaa ya Lindi na askari
hao kushiriki kutoa walichonacho kusaidia walemavu hao
Waandishi wa habari hufanya kazi kwa karibu na jeshi hilo hivyo
tunatarajia kupata Ushirikiano mkubwa toka kwa Kamanda Mzinga na
wasaidizi wake wakati wa matukio ya dharura na yasiyo ya dharura na
kuondoa hali ya Polisi wachache kuona Waandishi wa Habari ni maadui
wakubwa kutokana na maovu yao.
Mwaka jana Klabu ya waandishi wa habari ilifanya kazi vizuri na Jeshi
hilo, ilimalizia taarifaa ya LPC Iliyotolewa na Mwenyekiti wake Abdulaziz
Ahmeid ambae pia ni mwandishi wa Channel ten mkoa wa Lindi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...