Naibu
Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kebwe Kebwe amewataka
viongozi wa halmashauri kushirikiana na waganga wakuu kuhakikisha dawa
na vifaa tiba vinavyotolewa na Serikali kupitia Bohara Kuu ya Dawa MSD
vinatumika ipasavyo.
Dkt. Kebwe alisema hayo jana wilayani Masasi Mkoani Mtwara katika ziara ya kwanza toka uteuzi wake kutoka kwa Rais Kikwete wakati akiwa na kamati ya kudumu ya Bunge huduma za jamii kukagua taratibu za usambazaji dawa vituo na hospitali za Serikali.
Katika ziara hiyo amezitaka Hospitali za Serikali kutumia vyanzo vingine vya mapato ili kuweza kununua dawa na vifaa tiba katika kuongezea matumizi mbalimbali na bajeti ya Serikali.
“ni muhimu kuelewa kuwa hospitali inavyanzo vingi vya mapato wakati umefika sasa kutumia fursa hizo katika kuhakikisha mapato yanayotokana na vyanzo vya hospitali yanatumika pia katika kuongeza ununuaji dawa na vifaa tiba ili kuipa uwezo Serikali na jamii kufikia huduma ipasavyo”alisema
Naye Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge huduma za jamii Magreth Sita alisema ni muhimu suala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupewa kipaumbele cha hali ya juu kutokana na kuwa ndio msingi wa huduma bora za afya kwa jamii.
Alisema kutokana na ufanisi mkubwa uliopo katika upatikanaji dawa hospitalini na vituo vya afya baada ya mfumo wa ufikishaji dawa moja kwa moja hadi vituoni (DD) unaofanywa na MSD ni vizuri Serikali kutambua kuwa ufanikishaji wa hatua hiyo unahitaji uwezeshi hasa wa fedha za bajeti kufika kwa wakati.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya wadhamini MSD Dkt Ahmed Hingola alisema endapo Serikali itadhiti na kuhakiki dawa chache zilizopo ili kutekeleza mahitaji ni wazi lawama za wananchi kwa bohari ya dawa zitakwisha.

“MSD kazi yake kubwa ni upelekaji wa dawa huku usimamizi wa matumizi katika kutumika kama ilivyokusudiwa ikiwa bado ni changamoto hasa katika sehemu husika hivyo MSD imeanza harakati za uwekaji wa nembo dawa za Serikali (GoT) ili kudhibiti dawa hizo zisiweze kupita njia za panya”alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...