Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba akitoa hotuba yake wakati wa kufunga kongamano la siku tatu la uhamaji wa mfumo wa utangazaji kutoka Analojia kwenda Dijitali kwa Afrika (DBSF) 2014 katika Hoteli ya Naura Spring jijini Arusha. Kongamano hilo la 9 liliandaliwa na Shirika la Utangazaji kwa Nchi za Jumuia ya Madola (CTO) kwa ushirikiano mkubwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Srikali ya Tanzania ambao ndio wenyeji.
Mgeni rasmi katika ufungaji wa Kongamano hilo la DBSF 2014, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (wapili Kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (kushoto) Katibu Mtendaji wa CTO, Tim Unwin (wapili kulia) na Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka TCRA, Habbi Gunze.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (kulia) akizungumza kabla ya Mgeni rasmi kufungaji Kongamano hilo la DBSF 2014 katika Hoteli ya Naura jijini Arusha leo. Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (Kushoto), Katibu Mtendaji wa CTO, Tim Unwin (katikati) na Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka TCRA, Habbi Gunze. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...