Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe, (katikati) Mwakilishi wa Balozi wa Saud Arabia, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu, wakitiliana sahihi moja kati ya Hati za makabidhiano ya magari 20 aina ya Toyota Land Cruiser pamoja na pikipiki 40 vilivyotolewa na serikali ya Saud Arabia, vitendeakazi ambavyo vitasaidia katika kuongeza kasi na ufanisi katika kupambana na matukio ya uhalifu na wahalifu.(picha na Demetrius Njimbwi wa Jeshi la Polisi ).
Baadhi ya magari aina ya Toyota Land Cruiser yaliyotolewa na serikali ya Saud Arabia na kukabidhiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kupitia Jeshi la Polisi Nchini, magari hayo 20 pamoja na pikipiki 40 zenye thamani ya zaidi ya Dola Milioni moja huku magari hayo pamoja na pikipiki zikitarajiwa kupelekwa katika baadhi ya vituo vya Polisi hapa nchini ambavyo vinaupungufu wa vitendea kazi vya aina hiyo na kusaidia katika kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu.

 Baadhi ya aina ya Pikipiki zilizotolewa na serikali ya Saud Arabia na kukabidhiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kupitia Jeshi la Polisi Nchini, magari hayo 20 pamoja na pikipiki 40 zenye thamani ya zaidi ya Dola Milioni moja huku magari hayo pamoja na pikipiki zikitarajiwa kupelekwa katika baadhi ya vituo vya Polisi hapa nchini ambavyo vinaupungufu wa vitendea kazi vya aina hiyo na kusaidia katika kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu.(picha nap demetrius Njimbwi wa Jeshi la Polisi )

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. magari ya Jeshi la polisi inabidi yake na rangi uniform kuyatambulisha kama ni magari ya polisi sio kila magari ya msaada yana rangi yake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...