Moja ya mabango yaliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru nchini. Hafla hii ilifanyika muda mfupi kabla Rais Kikwete hajapanda ndege kuelekea London, Uingereza, kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kupanga mikakati ya kupambana na ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo na faru.
 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akibofya kwenye kompyuta kuzindua rasmi  mabango hayo ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru  kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Mahamoud  Mgimwa. 
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Far baada ya kuyazindua rasmi kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam 
 Moja ya mabango hayo likiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Farubaada ya kuyazindua rasmi kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk. Mahamoud  Mgimwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said  Meck Sadick.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mie nashauri hayo mabango yawe na neno za lugha za Kiingereza na Kichina,(wateja wakubwa wa hii biashala haramu) kutoa onyo kwa wageni hao wanaokuja TZ waelewe ni mwiko kuua wanyama.

    ReplyDelete
  2. Hivi swala ni mabango au majeshi yetu (polisi, JW, JWTZ, KMKM?, n.k.) kuamka na kwenda kazini??

    ReplyDelete
  3. Itakuwa ni ajabu ya kubadili usiku kuwa mchana kama serikali italisimammia na kufanikisha hili,kwani historia inatusuta.Kuna baadhi ya mambo mepesi ya kisheria ambayo either serikali iliamua kwa makusudi ku-turn the blind eye na kuyaacha yaendelee au ilinyoosha mikono ki aina kuashiria kushindwa kuyasimamia,hivyo hili nalo halitakuwa tofauti.Mfano;
    1.Swala la kuwaondoa wa machinga ktk maeneo wasiyorususiwa kufanya biashara.Ingawa hili liliwezekana kwa muda wakati wa ujio wa Obama.Leo hii Raisi huyu akifanya emergence landing Dar itakuwa ni aibu.
    2.Watu waliojenga ktk hifadhi ya barabara.
    3.Kuzuia magari yanayozidisha uzito kutumia barabara zetu
    4.Wauza unga etc..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...