Wanaharakati wakiwa na mabango wakiwa nje ya ukumbi  Lancaster House jijini London, Uingereza ambako  mkutano maalumu wa kupambana na tatizo la ujangili duniani  unafanyika leo. Rais Kikwete anahudhria mkutano huu maalumu  ambao umeandaliwa na Mwanamfalme wa Uingereza, Prince Charles.  Picha na Hans Pieter wa Globu ya Jamii, London.

Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara Haramu ya Wanyamapori 
(Conference on Illegal Wildlife Trade) unaanza rasmi leo katika 
ukumbi wa Lancaster House. 
Mkutano huu utakaohudhuriwa na jumla ya mataifa 47 na Mashirika 
13 ya Kimataifa umeitishwa na Serikali ya Uingereza kwa lengo la 
kujadiliwa na masuala maalum matatu kuhusiana na biashara 
haramu ya wanyamapori. Masuala maalum uyanayotarajiwa 
kujadiliwa ni Jinsi ya Kuimarisha Usimamizi wa Sheria (Law 
Enforcement) na mchango wa mfumo mzima wa sheria za jinai 
(criminal justice system) katika kukabiliana na biashara hiyo. 
Aidha, utajadili Jinsi ya kupunguza hitaji la bidhaa zinazotokana na 
wanyamapori (demand for wildlife products) na Jinsi ya kusaidia 
Maendeleo Endelevu kwa Jamii zilizoathiriwa na biashara hiyo 
haramu. 
Mkutano huu utazungumzia wanyama aina ya tembo, faru na tiger. 
Wanyama hawa wamechaguliwa kwa kuzingatia jinsi 
wanavyoshambuliwa zaidi na makundi ya wawindaji haramu kwa 
lengo la kuu pembe na ngozi zao. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete tayari ameshawasili Uingereza akiongoza 
ujumbe wa maafisa kutoka Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kushiriki 
Mkutano huu. 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hakuna Mtanzania hapo, we are either not pro-active, or oblivious of what is going on in our country, or both!!

    ReplyDelete
  2. Thank you so much for supporting us in this campaign against brutal killing of elephants for the benefit of the few senseless persons who want to get rich quickly.

    Tunawashukuru sana kutuunga mkono katika kampeni hii ya kuokoa tembo wetu kutokana na ujangili huu usiokuwa na imani kwa faida ya wachache wasio na huruma.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza nakubaliana na wewe. Unajua kwetu ukiwa Mmbongo ukisema cha maana unapuuzwa, lakini ukiwa ngozi nyeupe unaheshimiwaa, waache watusemee.Ndiyo maana kuna kamsemo ketu kale, "Nabii apendwi kwao". Fikiria majanga yaliyo sababishwa na watu miaka ya karibuni. Wenzetu wa nchi za huko viongozi wangejiuzulu mara nyingi tu, sababu wameshindwa,ingawa mala nyingine si kosa lao. Ndiyo kuwajhibika, siye tupo pale pale. Tukihesabu idadi ya Tembo walivyokuwa awali na sasa, ni wazi uongozi wote ungeachia ngazi. Kwani ni majanga na aibu. Na kesi ya ndugu zetu Alibino hivo hivo, mpaka Wazungu waliposimamia ilo swala hilo ndiyo ukaona haki za ulinzi wa watu unatendeka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...