Timu zikisalimiana
Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Kagera Sugar wakiikaribisha timu ya Rhino Ranger leo kutoka Tabora kwenye Ligi kuu ya Vodacom (VPL) wameifunga bao 1-0. katika mchezo huo ulio pigwa hii leo jumamosi katika kipindi cha kwanza timu zote mbili zilienda mapumziko zikiwa 0-0. Kipindi cha pili Kagera Sugar walifanya mabadiliko kwa kumuingiza mchezaji wao Seleman Kibuta na katika dakika ya 52 kipindi hicho hicho cha pili mchezaji huyo aliwapachikia bao la pekee. Bao hilo limepatikana baada ya kupigwa frii kiki na Hussein Mohamed(Shabalala) na kugonga posti upande wa juu na hatimaye Seleman Kibuta kuumalizia mpira huo ndani ya lango la Rhino Rangers.
Bao hilo limedumu mpaka dakika za mwisho wa kipute hicho na Kagera Sugar kumaliza mtanange huo na ushindi wa pointi tatu muhimu kwenye uwanja wao wa Nyumbani Kaitaba. Ushindi huu wa Kagera Sugar umewapandisha hadi nafasi ya tano wakiwa na pointi 26 huku Rhino Rangers wakiendelea kushika nafasi ya mwisho kwenye ligi hiyo wakiwa na pointi 13.
Picha ya waamuzi na timu kapteni wakiteta jambo muda mfupi kabla ya mtanange kuanza
Viongozi wa timu ya Rhino Rangers pamoja na wachezaji wa akiba
Sehemu ya Kagera Sugar, Viongozi na wachezaji wa akiba
Hivi chemsha bongo za 'Onyesha mpira ulipo' siku hizi hazipo tena?.Picha ya mwisho chini imenifurahisha,mchezaji namba 5 ameruka ameangalia upande mwingine,mpira huko nyuma yake.Mambo ya speed ya mwanga wa Camera na tukio.Si ndiyo ANKAL?
ReplyDeleteUwanja huo ufanyiwe ukaratabati kwenye sehemu ya kuchezea(nyasi ndefu sana)
David V