Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa Islamic Orphans,Halima Mpeta (kushoto),hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya kulipia ada za shule za watoto hao
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akiwapa vifaa vya shule watoto wa kituo cha TOVICHIDO.
Sehemu ya misaada hiyo ya vitu mbalimbali iliyotolewa na Kampuni ya Msama Promotions, kwa vituo vitatu vya watoto waishio katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa Islamic Orphans,Halima Mpeta (kushoto),akipkea msaada wa vitu mbalimbali kutoka katika mfuko wa Tamasha la Pasaka,Kutoka kwa Kampuni ya Msama Promotions Ltd.
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akimkabidhi kiasi cha shilingi laki saba Mlezi wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha TOVICHIDO,Honoratha Michael kwa ajili ya kulipia ada za shule za watoto hao.
======= ======== =========
Msama akabidhi misaada kwa vituo vitatu
KAMPUNI ya Msama Promotions waandaaji wa Matamasha ya Krimasi na Pasaka, jana ilikabidhi misaada mbalimbali kwa vituo vitatu vya jijini Dar es Salaam, ikitimiza ahadi ya kuisaidia jamii kabla ya Tamasha la mwaka huu linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama misaada hiyo iliyogharimu shilingi milioni 7 imekabidhiwa katika vituo vya TOVICHIDO cha Temeke Maganga, Malaika Kids cha Mwananyamala na kituo cha Yatima cha Mwandaliwa.
Msama alisema katika sehemu ya msaada huo pesa taslim shilingi milioni 2.9 ni ada kwa wanafunzi na nyingine ni kwa vifaa mbalimbali yakiwemo madaftari, sabuni za mche, unga, mafuta ya kupaka na sukari. Aidha Msama alisema misaada hiyo imetokana na mfuko wa Tamasha la Pasaka kama ilivyokuwa kwenye Tamasha la Krismasi ambalo walikabidhi misaada ya shilingi milioni 4.
Mkurugenzi wa TOVICHIDO, Honarata Michael alimpongeza Msama kwa kuwajali watoto na jamii kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa kituo cha Mwandaliwa, Halima Mpeta alisema anamshukuru Msama kwa kujali jamii kwani katika kituo chake si mara ya kwanza kukisaidia na amezidi kumuomba aendelee na moyo wa kukisaidia kituo chake na vingene vyenye mahitaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...