Katibu Mkuu wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Aspiration Initiatives - TAI Bw. Gwamaka Mwabuka akitoa maelekezo kwa mwanafunzi wa darasa la pili shule ya Msingi Kilimani Juma Abdul jinsi ya kunawa mikono kwa usahihi ili kuipeka magonjwa. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wanafunzi toka Denmark waliopata mualiko na TAI kupitia taasisi ya Global Platform. 
  Wanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Kilimani wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kusafishwa kinywa na kuepukana na magonjwa yanayotokana na kutosafisha kinywa.
1Baadhi ya wanafunzi w shule ya awali ya Kilimani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waliowatembelea kuwafundisha swala zima la usafi shuleni hapo kupitia miradi ya Mikono Ming’avu (MiMi) na Kinywa Kisafi (KiKi) chini ya Taasisi isiyo ya kiserekali ya Tanzania Aspiration Initiatives – TAI. 

=========      ==========   ==========

TAI YATOA MAFUNZO KWA VITENDO JUU YA KUNAWA MIKONO NA KUSAFISHA KINYWA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KILIMANI JIJINI DAR ES SALAAM

10 Februari, 2014, Dar es slaam, Tanzania

Taasisi isiyo ya kiserikali ya TAI - Tanzania Aspiration Initiatives imefanya mafunzo ya kulinda afya kwa vitendo kwa wanafunzi Zaidi ya 200 wa Darasa la Kwanza, la pili na darasa la awali katika shule ya msingi Kilimani iliyopa Sinza Uzuri wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa miradi miwili inayojulikana kama Mikono Ming’avu (MiMi) na Kinywa Kisafi (KiKi).

Miradi yote ina lengo kuu la kupambana na magonjwa yanayoweza kuzuilika kama Magonjwa ya tumbo na yale ya meno na kinywa yanayoathiri zaidi watoto. Mafunzo hayo pia yalishirikisha Vijana wengine kutoka nchini Denmark walio nchini katika ziara ya kimasomo chini ya Jukwaa la kimataifa la Global Platform.

Mikono Ming’avu (MiMi) ni mradi uliyojikita katika kutoa mafunzo kwa vitendo kwa watoto wa shule za msingi kutatua tatizo la magonjwa yanayosababishwa na mikono michafu kama vile Pneumonia na homa ya Matumbo (Diarrhea). Mradi huu tayari umeshawafikia Zaidi ya watoto 1000 katika baadhi za shule za msingi jijini Dar es salaam huku malengo ni kufikia shule zote za msingi Tanzania nzima.

"Hatua hizi za TAI ni baada ya kuona Watanzaia wengi hawana tabia ya kunawa mikono na sabuni kwa ufasaha ambapo ni moja ya sababu inayochangia magonjwa yanayoweza kuzuilika, lakini pia yanaathiri ukuaji wa mtoto. Kila mwaka watoto Zaidi ya milioni 3.2 duniani walio chini ya miaka 5 wanakufa kwa sababu ya homa ya matumbo na pneumonia yakiwa ni magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo kwa watoto baada ya malaria hasa katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara, Tanzania ikiwepo" alisema Bw. Gwamaka Mwaibuka, Katibu Mkuu wa TAI. 

Kinywa Kisafi (KiKi) ni ni moja kati ya mradi ya TAI ukiwa na lengo la kupunguza tatizo la magonjwa ya Kinywa na meno kwa watoto ambapo taasisi hiyo hufanya mafunzo kwa vitendo kwa kushirikiana na wataalam kuwafundisha watoto njia sahihi za kufanya usafi wa meno na kinywa na kuhimiza tabia ya kusafisha kinywa kuanza tangu utotoni.

TAI ni taasisi iliyoanzishwa kwa lengo la kuimarisha maisha ya kila mmoja katika jamii hasa watu wanaoushi katika mazingira magumu na umasikini kupitia sekta tano za Elimu, Afya, Ujasiriamali, Teknolojia ya Habari na Mazingira. Kwa taarifa Zaidi ingia www.tai.or.tz au Tufuate katika ukurasa wetu wa Facebook www.facebook.com/tai2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...