Uncle tumekua tukilia kilio cha muda mrefu huku kwa Ali maua Kijitonyama kuhusu tatizo la Maji, mara ya mwisho tumepata huduma hii wiki tatu zilizopita.
Ila kwa sasa matatizo yetu yameongezeka maana kwa muda wa siku tatu sasa tunalala usiku bila ya huduma ya umeme na mchana tunaupata kwa mgao.
Kwa kweli wakazi wa maeneo haya tunateseka sana na huduma hizi mbili na hakuna maelezo yeyote kutoka kwa wahusika.
Tunaomba mawaziri husika watusaidie kama sio kupata huduma hizo basi angalau maelezo ya kwanini na mpaka lini?
Mdau.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...