Mwaka 1994: Rais Ali Hassan Mwinyi akiwa na wajumbe wa kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde Ikulu jijini Dar es salaam baada ya timu hiyo kunyakua ubingwa wa Chalenji. Kutoka kulia mstari wa mbele ni Ankal, Brigedia Moses Nnauye (RiP), Mwenyekiti wa FAT Alhaj Muhidin Ndolanga, Rais Mwinyi, Waziri wa Elimu na Utamaduni Profesa Philemon Sarungi, Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Reginald Mengi, Mbunge wa Dodoma Kuwayawaya S. Kuwayawaya na Kamanda Richard Mwaikenda. Toka wakati huo Taifa Stars haijashinda kombe lingine lolote... Kulikoni?
Home
Unlabelled
Kutoka maktaba: Mzee Ruksa na kamati ya saidia taifa stars ishinde mwaka 1994 na wanahabari Ikulu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ankal na shati la uji uji enzi zile wa acha tuuu
ReplyDeleteancal wamechukua chalenge juzi juzi kombe nafkiri tuliwafunga uganda nikija kwenye swala lako sababu ya kuwa hatuna timu.nzuri ya taifa sababu kuu ligi yetu haina ushindani pili tim kubwa zinanunua mechi tatu wachezaji wetu hawajitumi.na wananunulika wanakatisha tamaa mchezaji anapata tim france eti anagoma aje acheze ligi ya fitna tofauti na wachezaji wa africa maghribi ukiskia njia walozopitia kwa wachezaji wetu hawawezi hata siku moja leo wanatamba ulaya
ReplyDeletejengine ancal kama tunataka tim yetu ya taifa iwe nzuri tuige leo simba na yanga zinaweza zikacheza taifa mechi suta mfululizo wakati hizo tim nyengine zina viwanja vyao hapa hapa dar na mlandizi jambo jengine walim hawana sifa za kufundisha ligi kuu wadhamin nao tatizo marefaa nao tatizo watendaji wa tff nao wana usimba na uyanga waandishi wa habari nao wanashindwa kuzuia hisia zao badala yake ukweli hawausemi lazma tubadilike viongozi wa simba na yanga wako kutaka umaarufu kuliko maslahi ya hivi vilabu
ReplyDeleteAnkal Kiboko...umetaja msitari wa mbele tu!!!!! Duh!!!!
ReplyDeleteNdiyo umuhimu wa kupiga picha za kumbukumbu ukichelewa kidogo unakuwa umezeeka.
ReplyDeleteMdau wa#2 nakubaliana na wewe. Siye kwetu hawajui jamaa wa Africa ya Magharibi wanafanya wanapitia matatizo ghani kufikia kucheza Ulaya na Marekani. Mie mwalimu wa Mpira huku, wacheza wengi toka Bongo wanaomba kuja kujaribisha, lakini ni kweli shughuli zenyewe hatuziwezi. Kujaza maforms kwa muda, hali ya hewa(sana baridi), Vyakula,tabia,Lugha, safari ndefu, hamna ndugu, na mala nyingi ni mweusi pekee n.k Ukiangalia wacheza wengi wa Africa wanaotamba kwenye hizi ligi za Ulaya, wengi walikuja wakati wadogo na walio wakubwa wamepitia matatizo mengi. Mfano, karibu timu yote ya Nigeria chini ya miaka 17 wanachezea vyuo vya Marekani kwani timu yao inakuja kila mwaka kucheza Dallas Cup. Au George Weah Opong alipelekwa Brazil na serikali yake akiwa mdogo. Jamaa aliye goma jwenda Ufaransa inaweza kuwa kati ya hizo sababu au vipimo. Vile vile unweza kuwa mchezaji mkubwa Bongo lakini Mataifa ya Magharibi ni wakawaida tu na upati namba. Kuna wacheza wakali sasa hivi Yanga ambao Marekani walikuwa wanakula benchi dalaja la tatu. Lakini kila mtu na bahati yake, kama Nonda, alitoswa Yanga lakini Italy alikuwa ndiyo mkali.
ReplyDelete