Ofisi ya Rais - Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (OR- UUM) imetoa taarifa kwa umma kuwa utekelezaji wa mfumo wa – Big Results Now ! (BRN) unaendelea vizuri. Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaweka utaratibu thabiti wa kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa miradi katika maeneo sita ya kimkakati kitaifa (Kilimo, Elimu, Maji, Nishati , Uchukuzi na Utafutaji wa Rasilimali).

Mfumo wa BRN unaweka wazi malengo pamoja na kuainisha uwajibikaji kwa kila mshiriki mmoja au taasisi katika utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kupata mafanikio haraka.

Kila Wizara inayotekeleza mfumo huu imeanzisha Kitengo cha Kusimamia Utekelezaji (Ministerial Delivery Unit (MDU)) ambacho kinafanya kazi kwa karibu sana na OR-UUM.

Majukumu ya MDU ni kufuatilia na kuthamini utekelezaji wa miradi wa kila siku na kuanda taarifa za utekelezaji za kila wiki na mwezi ambazo huwasilishwa OR-UUM. 

Taarifa za MDU zinajadiliwa kila mwezi kwenye mikutano ya Kamati ya Wizara ya Kusimamia eneo la kimkakati Kitaifa (Steering Committee Meetings) ambayo Mwenyekiti ni Waziri wa Wizara husika pamoja na Baraza la Mageuzi na Ufuatiliaji Utekelezaji ambalo Mwenyekiti ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Mikutano hii inalenga kutatua changamoto Aidha, Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha Vitengo vya Kusimamia Utekelezaji katika ngazi za Mikoa (Regional Delivery Units - RDUs) pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Council Delivery Units - CDUs) ili kuongeza Bwana Omari Issa, Mtendaji Mkuu wa OR- UUM alisema, “Tanzania ina mawazo makubwa na Dira na mipango sahihi ya kuleta maendeleo. kinachokosekana ni mfumo sahihi wa kufuatilia utekelezaji ili kupata matokeo yaliyolengwa.

BRN inaondoa dosari hii. Aidha, BRN inaleta mageuzi ya uwajibikaji katika ngazi zote Ili kufanikisha BRN, tunahitaji kupata ushirikiano kutoka sekta binafsi ambayo italeta teknolojia, utaalum wa menejimenti na mtaji.

Ili kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi, BRN imeanza mchakato wa kurazinisha mfumo na taratibu za ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili tuhakikishe kwamba sekta binfasi inatoa mchango wake stahiki katika kutekeleza BRN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. The mdudu,,hongera sn serikali kwa kuja na mipango kabambe na imara kama hiyo,,kwa mipango hiyo tutaona sasa tunakoelekea kuzuri coz uongozi si dili tena bali ni moto mkali,,mitendaji mizigo nayo itawajibika hivyo ndivyo nchi inavyotakiwa kuongozwa na sivinginevyo,,nilikua na mpango wa kususia idara zote za kiserikali lakini kwa mipango hiyo NASITISHA MPANGO WANGU na kua bega kwa bega na serikali yangu,,coz ilikua inaniuma sn moyoni kuona SHULE HAZIFANYI VIZURI,MAHOSPITALINI ndio usiseme akina mm na madada zetu wakijifungulia chini ya sakafu,VIWANDA VYA MAANA hatuna wakati tuna kila aina ya MATUNDA Mifugo,DHAHABU kila aina tunazo,USAFIRISHAJI NJIA ZA RELI ZA KISASA HATUNA,,TOWN ZA MAANA HATUNA wakati tuna shilika zuri la nyumba,,ngoja niishie hapa maana naandika huku nikitokwa na machozi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...