·        Je  wewe  ni  kijana  wa  kitanzania?
·       Una  umri  wa  kuanzia  miaka 15  na  kuendelea ?
·       Una  ndoto za  kuwa  muigizaji filamu  mkubwa  nchini  Tanzania?
·       Una  ndoto  za  kuwa  mwanamuziki ama  muimbaji  mkubwa hapa  Tanzania ?
RAFIKIELIMU  MUSIC &FILM  ACADEMY   ni  kituo  kinachotoa  mafunzo  ya  UIGIZAJI  na  UIMBAJI  kwa  vijana wa kitanzania  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  kumi  na  tano na  kuendelea.
Wahitimu  wa  mafunzo  haya  hupata  nafasi  ya  kushiriki  katika  filamu , maigizo, tamthiliya  na nyimbo mbalimbali   zinazo  tayarishwa  na Taasisi  ya   RAFIKIELIMU  FOUNDATION.

ADA  YA  MAFUNZO :  Mafunzo  haya  hutolewa BURE!
Mafunzo  yataanza rasmi  tarehe  02 MACHI  2014.
Mwisho  wa  kujiandikisha   ni  tarehe  28 FEBRUARI 2014.
Chuo  chetu  kinapatikana  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU mbele  ya  CHUO  KIKUU  CHA  DAR  ES  SALAAM.
Kufika  Chuoni  kwetu, panda  daladala za  UBUNGO-CHANGANYIKENI  kisha  shuka  katika  kituo  cha  TAKWIMU  halafu  tembea  hatua  ishirini  mbele, utaona  bango  limeandikwa  RAFIKIELIMU  FOUNDATION.

JINSI  YA  KUJIANDIKISHA :Tuandikie  barua  pepe  kwenda :  rafikielimutanzania@gmail.com    
Kwa  maelezo zaidi, wasiliana  nasi  kwa  SIMU
0784406508   
Au  Tembelea  
                www.rafikielimu.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...