Demokrasia vijijini itapatikana iwapo vyombo vya habari jamii vitatumika kikamilifu na kutekeleza wajibu wake wa kupasha habari kwa kutumia teknolojia mpya.
Akifungua mafunzo ya wiki moja katika Ukumbi wa Mazingira, Kibaoni Ifakara yanayowashirikisha wanahabari jamii kutoka Pemba, Unguja, Pangani, Ifakara na Kyela, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Hassan Masala amesema mbinu za kisasa zinahitajika kuelimisha jamii na mambo gani yafanyike ili kupata uongozi bora vijijini na taifa kwa ujumla.
Mkufunzi wa Teknolojia ya simu kwa habari kutoka Chuo Kikuu Bibi Faith Shayo akifafanua jinsi simu za “SMART” zinavyoweza kutumika kwa habari mbalimbali, picha na maoni kutoka na kwenda katika jamii kupitia maelekezo husika yaliyomo katika simu.
Bwana Masala amesema pamoja na changamoto zilizoko vijijini, Redio Jamii Pambazuko iliyoko Ifakara, ina mchango mkubwa katika kuelimisha na kukuza demokrasia katika wilaya ya Kilombero kwa kuwa inafika sehemu kubwa ambako serikali haifiki kwa urahisi.
Amesema kutokana na miundo mbinu mibovu ya usafiri, mafunzo ya matumizi ya simu kwa kiasi kikubwa yataongeza ujuzi katika taaluma ya upashaji habari.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 7 mwezi Februari 2014 yanalenga kutambua uwezo wa simu katika kutafuta na kutoa habari, kujifunza jinsi Tehama inavyorahisisha mawasiliao kwa njia ya simu aina ya “SMART” na kuboresha mbinu za upatikanaji na utoaji wa habari.
Mafunzo ya Tehama kwa redio jamii ni mwendelezo wa mradi wa kuzipatia uwezo redio hizo kwa kutumia teknolojia mpya unaofadhiliwa na UNESCO kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA).
Mkufunzi na Mtaalamu wa Masuala ya Redio Jamii Mama Rose Haji Mwalimu kutoka UNESCO, akieleza madhumuni ya mafunzo kwa washiriki, katika Ukumbi wa Mazingira Kibaoni, Ifakara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...