Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya(wa pili kulia) akielezea hatua mbalimbali za Maandalizi ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga(wa kwanza kulia) ni Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Mkaguzi wa Magereza Deodatus Kazinja alipotembelea kujionea hatua mbalimbali za ukarabati unaoendelea leo Februari 7, 2014 Jijini Tanga.
Muonekano wa mbele wa Jengo la Kikoloni ambalo linalotarajiwa kukarabatiwa kwa ajili ya Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga. Jengo hilo hapo awali lilitumika kama Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Tanga ambapo hivi sasa Jeshi la Magereza tayari limeanza ukarabati wa jengo hilo. Wa kwanza katika picha ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya akiwa ameongozana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza leo Februari 07, 2014 Jijini Tanga.
Tofali ambazo zimefyatuliwa kwa ajili ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga. Ukarabati huo wa Ofisi mpya za Utawala unaanza hivi karibuni Jijini Tanga na utasimamia kwa karibu na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya akiongoza Kikao kazi Ofsini kwake pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wanaofanya kazi Ofisi ya Magereza Mkoa wa Tanga leo Februari 07, 2014 alipotembelewa Ofsini kwake na timu ya Maafisa Habari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaaam(hawapo pichani)
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wanaofanya kazi Magereza Mkoa wa Tanga baada ya kutembelea sehemu mbalimbali ya maandalizi ya ukarabati wa Ofisi Mpya za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga leo Februari 07, 2014(wa Nne kulia) ni Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Augustino Mboje(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...