Kikosi cha Twiga Stars kinashuka Uwanja wa Nkoloma, Lusaka nchini Zambia leo kuwavaa wenyeji Zambia (Shepolopolo) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayooneshwa moja moja ‘live’ na televisheni ya Shirika la Taifa la Utangazaji la Zambia (ZNBC).

Mechi hiyo itaanza saa 9 kamili mchana kwa saa za Zambia ambapo Tanzania itakuwa saa 10 kamili jioni huku Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage akiwa tayari ametangaza ‘silaha’ zake kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza.

Watakaoanza kupeperusha bendera ya Tanzania katika mechi hiyo ambayo kiingilio ni bure kwa majukwaa yote isipokuwa lile kuu ni; Fatuma Omari 1, Fatuma Bashiru 17, Donisia Daniel 2, Fatuma Issa 5, Evelyn Sekikubo 15, Sophia Mwasikili 16, Vumilia Maarifa 10, Mwapewa Mtumwa 9, Asha Rashid 14, Etoe Mlenzi 13 na Shelida Boniface 7.

Wachezaji wa akiba ni Maimuna Said 18, Fatuma Hassan 12, Zena Khamis 6, Esther Chabruma 8, Amina Ally 4, Therese Yona 11 na Happiness Hezron 3.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...