Na Abdulaziz Video,lindi
Kampeni za Uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kiwalala umefungwa na
Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Bernard Membe kwa kuwataka
wananchi wa kata hiyo kutofanya makosa kwa kumchagua ndg Zahoro
Shineni
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama mkoa wa
Lindi akiwemo katibu mkuu wa Umoja wa Vijana Taifa pamoja na Viongozi
wa CCM wa mkoa wa Mtwara waliokuwa wakielekea katika kufunga kampeni
za Uchaguzi Mdogo Huko Mkwiti Mkoani Mtwara
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe akimnadi Mgombea wa Udiwani wa kata ya kiwalala kupitia CCM, Zahoro Shineni Hamis katika mkutano wa kufunga Kampeni uliofanyika katika kijiji cha Mahumbuka Lindi Vijijini
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Taifa,Sixtus Mapunda akiwaasa Wananchi wa Kiwalala kumchagua Mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Kiwalala
Moja ya Burdani zilizotolewa na wasanii katika kufungwa kwa kampeni za CCM
Mbunge wa Jimbo la Kilwa kaskazini, Mhe. Murtaza Mangungu akimuombea kura mgombea wa Udiwani katika kijiji cha kiwalala
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...