Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinti, akizindua huduma mpya ya PSPF Pamoja nawe na PSPF call centre, itolewayo na mfuko wa Pensheni wa PSPF, baada ya kufungua Mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo Feb 26.2014.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (kushoto), akimkaribisha mjumbe wa bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ambaye pia ni katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimatifa, John Haule alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimtaifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, kuhudhuria mkutano mkuu wa tatu wa Mfuko wa PSPF wa wadau Februari 26.2014.
Wakurugenzi wa idara mbalimbali za mfuko wa Pensheni wa PSPF, mstariu wa mbele, wakiwa miongoni mwa wajumbe wanaohudhuria mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo Februari 26, 2014
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akishuka kwenye gari lake, huku naibu waziri wa fedha, Adam Malima (kushoto), akiwa tayari kumpokea kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo, kufungua Mkutano Mkuu wa Tatu wa Wadau wa mfuko wa pesnheni wa PSPF.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...