Mkuu wa mkoa wa Lindi na ujumbe wake wakikagua Zahanati ya Kijiji cha Kikulyungu wilayani Liwale
Nyumba ya wahudumu wa Afya kijiji cha kikyulungu inayojengwa kwa Msaada wa Benjamin Mkapa Foundation
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Ludovick Mwananzila (mwenye suti ya kijivu) akikagua miradi ya Maendeleo wilayani Liwale
Mkuu wa mkoa wa lindi MheLudovick Mwananzila akihutubia wananchi wilayani liwale kulia ni mkuu wa wilaya ya Liwale Mhe. Ephraim Mmbaga
Mkuu wa mkoa wa Lindi akikagua ujenzi wa maabara shule ya sekondari Nicodemus Banduka
wilyani Liwale. Picha na habari na Abdulaziz Video.
-----------------------------------------
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Ludovick Mwananzila ametoa siku saba kwa wazazi
na walezi wote kuwapeleka shule wanafunzi waliochaguliwa na
kutakiwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu 2014.
Agizo hilo amelitoa kwa nyakati tofauti wakati anazungumza na
wananchi wa kata ya Kikulyungu, Barikiwa, na Mpigamiti alipokuwa
kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo wilaya himo.
Mhe. Mwanazila alisema elimu ni suala muhimu kwa mtoto ambalo
halitakiwi kufanyiwa mchezo hivyo basi mzazi,mlezi atayekaidi agizo
hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa pamoja
na kufikishwa mahakamani.
Alisema maendeleo hayawezi kupatikana kila ya elimu hivyo basi elimu
ndiyo msingi wa kila jambo kwa kulitambuan hilo ndiyo maana serikali
sikivu imeanzisha mpango wa shule za sekondari za kata nchini.
Awali mkuu wa wilaya Liwale Mhe. Ephraim Mmbaga alisema katika wilaya
yake wanafunzi 1154 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari
mwaka huu lakini hadi sasa wanafunzi 482 tu waliofika katika shule
walizopangiwa
Mhe Mmbaga alisema wanafunzi 672 hawajafika shuleni kwa sababu ambazo sio
za msingi hali ambayo inatishia na kukatisha tamaa katika ustawi wa
maendeleo ya elimu wilaya humo,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...