Habari za leo ndugu, ninakuomba unisaidie kuweka waraka wangu kwenye blogu yako, ili watu wenye uwezo wa kunisaidia hata kwa ushauri tu, waweze kunisaidia kwani nipo katika wakati mgumu sana sasa hivi  Natanguliza shukurani zangu za dhati kwako.

Kwa ufupi mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 26 . Ninaishi Dar Es salaam na kazi yangu ni mfanyabishara. Baada ya maisha kunipiga sana, niliamua kwenda kuomba ushauri kwa mdada mmoja jirani yetu ambaye yeye mambo yake yalikuwa yamemnyookea sana.

Dada huyo aliniunganisha na mmama mmoja ambaye alikuwa anaishi Masaki, mama huyo akanipeleka kwenye klabu ya wanawake wasagaji ambao ni matajiri ambako niliingizwa kwenye utaratibu wa ibada (matambiko ) yao. Hekalu la wanawake hawa matajiri lipo katika wilaya ya Kinondoni.

Waganga wakuu wa hekalu hilo wapo watatu, kuna wanaume wawili ambao ni vijana vijana tu na mwanamke mdada mmoja ambaye yupo kwenye umri wa kama miaka arobaini hivi na ushee.

Watu hawa watatu ni wachawi wenye nguvu za ajabu sana na pindi unapojiunga na klabu hii, unakula kiapo cha kutii na kufuata masharti yao katika siku zote za maisha yao. Wanao kiuka masharti yao huwa wanapata matatizo makubwa sana.

Katika hekalu hilo, zinafanyika ibada za uchi za kila mwisho wa wiki na huwa zinahusisha mamia ya wanawake. Niliingia katika klabu hii tangu mwaka jana (2013) mwanzoni, kweli nilipoingia nilitajirika sana baada ya muda mfupi tu. Kila kitu nilichokitaka katika maisha yangu nilikipata.

Hata hivyo pamoja na kupata mali na utajiri kupitia klabu hii, mimi ninataka kujitoa ingawa nashindwa kwa sababu naogopa kupata adhabu ya kuvunja kiapo cha watu hawa.

Ninataka kujitoa kwa sababu, kwanza sina amani moyoni mwangu. Nafsi yangu inanisuta sana kupata mali ambazo zinatokana na kujiunga na klabu ambayo memba wake wanamuabudu shetani, vilevile ninajiona mkosaji sana kwa ninacho kifanya kwa sababu ni kama nimekuwa muabudu shetani.

Tatizo linalo nikabili ni kwamba, ninataka kujitoa lakini ninashindwa kwa sababu ninaogopa kupata adhabu ya kukiuka masharti ya klabu( dini ) hii ambayo kwa kweli ni magumu sana kwangu.

Ni tamaa tu ndio iliyo niponza, naomba mnisaidie ndugu zangu japo hata kwa kunipa ushauri. Vilevile ninawasihi akina dada wa hapa Dar Es salaam, ambao nawaona kwa wingi sana wanaingia katika klabu hii.

Kuweni makini sana wadada wenzangu, hakuna hela wala mali za bure, kila kitu kina gharama yake, utakapo fika wakati wenu wakulipa gharama zake, mtakielewa ninacho kizungumzia hapa.

Nipeni ushauri kupitia barua pepe yangu ambayo ni : tunukondo@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Mrudie Mungu, nenda kwenye kanisa lenye nguvu za Mungu, simulia hadithi yako, utaombewa, utafanyiwa deliverance, utaelekezwa jinsi ya kuenenda na Mungu na jinsi ya kumshinda shetani. Hamna uchawi wenye nguvu mbele za Mungu. Kwani huyo shetani si ni kiumbe tu kilicho ubwa na Mungu? Ka mreport shetani kwa muumba wake haraka sana atashikiswa adabu.

    wala usiogope.

    ReplyDelete
  2. Pole saaana binti Tunu!!! Umeingiwa na hofu tuu hakuna lolote litakalo kupata, ni kweli hao watu wapo na serikali inajuwa lakini kwa uhuru wa kuabudu wanachokifanya sio kosa kisheria. Ningependa nikushauri tuu kuwa hii dunia haina mwenyewe, isipokuwa wewe endelea na huo mzunguko hadi siku yako ya mwisho, kwani hapa duniani kila linalomkuta mwanaadamu lilisha pitishwa na muumba wako, kwani ingekuwa mwanaadamu anajipangia aweje usingefika huko, na kwa nyongeza wewe nenda huko kama mwanachama usifikirie udini kwani dini za dunia hii tuliomo ni kama vyama vya siasa hamna ukweli ni ulafi na uchoyo tuuu, ni sawa na wabunge wanaodai posha badala ya umuhimu wa katiba, enzi zetu sisi hatukuwahi kusikia wabunge wakilumbania posho. Mimi nakushauri uendelee hukohuko hakuna ibada ya shetani wala ya ibilisi ONDOWA SHAKA HAYO NDIO MAISHA UMEJALIWA NA MOLA WAKO.

    ReplyDelete
  3. Kwa Mungu kila kitu kinawezekana, usiogope viapo ulivyopewa bila kujali utapatwa na nini. Ni bora ubaki na maisha magumu lakini uwe huru. Yesu bado anakupenda na atakuweka huru.

    ReplyDelete
  4. ANAHITAJI MAOMBI NA USHAURI WA KIMUNGU PLUS JINSI WATU WENGI WAMEFANIKIWA KUTOKA HUKO. ITS POSSIBLE KUTOKA HUKO MUNGU ATAFANYA NJIA YAKO KUWA RAHISI.

    0766192827

    ReplyDelete
  5. Jitowe tuuu, hayo masharti ni myth tu. Kwani umepata adhabu gani kwa kulikisha habari hii michu blog?

    ReplyDelete
  6. Amen, jibu lako ni Mungu. Mrudie Mungu wako na utaokolewa katika hilo janga. Piga moyo konde na uchukue hatua.

    ReplyDelete
  7. Pole sana, lakini kitendo cha kujisikia vibaya kumuabudu shetani, ni hatua nzuri na bado Mungu anakupenda ndo maana unajisikia vibaya, nafsi yako bado i hai, maana nafsi ikishakufa, usingesikia chochote. Nakukaribisha katika Huduma ya Madhabahu ya Maombezi ya Mwili wa Kristo, iliyopo kinondoni Mannyanya, piga namba hii kwa maelekezo ya namna ya kufika,nakuhakikishia hakuna pepo wala shetani ambaye atakuweza baada ya kuja katika madhabahu hii, utaombewa, Yesu ataingia ndani yako, na roho mtakatifu atakuwezesha na wachawi wote hawatakuweza kabisa. Piga namba 0658 322 925 kwa maelekezo ya namna ya kufika kanisani. Hii ni namba ya kanisa.

    ReplyDelete
  8. haha haha... Michuzi sikuwa najua kama siku hizi unaruhusu mikasa ya kubuni.

    Huyu jamaa knichekesha kweli kweli kwanza kasema ni wasagaji matajiri halafu anahadithia kuwa ni wacawi na kucheza uchi, toka lini hayo yakawa ni usagaji? huo ni ushirikina tu. Inaonyesha hata kashindwa kumaintain stori yake aidha ni wasagaji au ni wachawi wanaocheza uchi kila wiki?

    Halafu anadai anaogopa kutoka na pia anaogopa tishio la kupata matatizo kwa kuepuka masharti yao, lakini wakati huo huo ametoa bayana muda aliojiunga, kama kweli kundi hili lipo na wanataka kumjua huyu aloleta habari hii hapa si watamjua tu kwa kuangalia ni nani aliejiunga muda huo.

    Mwisho nimefurahi kuona hadithi za kubuni kama hizi zimeanza kuweka katika blog hii

    ReplyDelete
  9. ALIYEKUUMBA ANANGUVU KUBWA SANA KULIKO YEYOTE YULE.

    UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUMWAMBIA ALIYEKUUMBA NISAIDIE; UFANYE HIVYO KWA MOYO WA DHATI.

    YANI SEMA HIVI "EE ULIYENIUMBA MIYE NA WENGINE, NA ULIYEUMBA HII DUNIA NA VIUMBE VYAKE, ULIYEUMBA ARDHI NA MBINGU, NA ULIYEUMBA KILA KILICHO HAI NA KISIHOHAI; NAJILINDA KWAKO NA SHARI ZITOKANAZO NA BINADAMU NA MAJINI, NAJILINDA KWAKO NA KILA LILO NA SHARI. EE ULIYENIUMBA NISAIDIE KUONDOKANA NA MATESO HAYA NINAYOYAPATA".

    USEME HIVYO MARA TATU ASUBUHI NA MARA TATU BAADA YA JUA KUZAMA. NA KWA KUWA HUIPENDI HIYO KAZI, UNATAKIWA KUACHA MARA MOJA NA UDHAMIRIE KUTOTENDA TENA. HAKIKISHA UNACHUKUA ULINZI KUTOKA ALIYEKUUMBA.

    NI HIVYO TU, ALIYETUUMBA AKIPENDA ATAKUSAIDIA. HAKIKISHA USICHANGANYE NA KITU CHOCHOTE NI HAYO MANENO TU YANATOSHA; MANAKE WENGINE WATAKUELEWA UENDE KWA MSUKULE SIJUI KWA MGANGA WA NIJERIA SIJUI KWA KUPIGA RAMLI; HAYA PIA NI MAMBO YA SHETANI.

    MUUMBA AKUONGOZE KATIKA HAKI NA AKUSAIDIE.

    ReplyDelete
  10. Kama ni muislam lete istighfar ya nguvu,sala za usiku kwa wingi,tembea na udhu muda wote,acha hiyo mali uanze upya na ili kuwaokoa kinadada wengine katoe taarifa ktk vyombo husika.kwa Allah hakuna linaloshindikana

    ReplyDelete
  11. The mdudu,mtumeee yaani tanzania yetu imefika mahara hapa? I cant biliivu hii kitu kama kweli ipo ndani ya nchi yetu,sasa tujiulize haya maswali hivi ni nn maana ya kazi za polis jamii? Au polis wenyewe hasa,pia vipi ujirani mwema hivi haupo tena hapo tanzania? Coz mwezenu kama nilivyosema hapo siku za nyuma ya kwamba NIMESEPA SIKU NYING SN ila kila nikifuatilia mambo ya huko mengi ni ya AJABU AJABU 2,yaani tanzania ya leo kama iko juu ya anga inaelea elea vile bado tu kudondoka,why nasema hivi? 1 watu wamependekezwa na makundi yao na kisha RAIS wetu kawateuwa ili wakatutengenezee KATIBA YENYE TIJA KWA TAIFA NA WATU WAKE lakini cha ajabu hao watu chakwanza kabisa walichokiona ni POSHO ndugu zangu mm nilistuka sn,2 kuna huyu mama ambae ni PROFESA nimemuona kwenye kipindi cha WANAWAKE LIVE yaani mama ameongea vitu vya maana sn coz hata mm binafsi sikubaliani na hao watu wanaopinga haki za akina mama na watoto pamoja na wazee so inasikitisha sn huyu mama hawampi ushilikiano wa kutosha kuhakikisha kwenye katiba mpya kinawekwa kitengo maarumu cha kufuatilia kwa ukaribu hizo haki za akina mama na watoto pamoja na wazee wetu,hatutaki kusikia tena akina mama na madada zetu wakipoteza maisha yao wakati wa KUJIFUNGUA nasema haikubaliki hata siku moja,ninamengi ya kuongea but wacha niishie hapa kwa leo.

    ReplyDelete
  12. Shetani mbona unawatesa wanadamu kwa jina la utajiri! Nenda kanisani ukaombewe. Mungu ni mwema, atafanya njia ya kutokea na atakuweka huru katika maisha yako. Amini kwamba yeye ni BWANA asiyeshindwa, utapona.

    ReplyDelete
  13. Kamshitaki shetani kwa BWANA YESU ndio dawa pekee.

    ReplyDelete
  14. Amua, ukiamua kwa dhati Mungu atakuwezesha.

    ReplyDelete
  15. Kwa sababu makanisa ni mengi na mengine hayashughulikii ukombozi ushauri ni nenda Agape International kwa Fernandes Mbezi kwa kuendeleza maonbi.Ushauri wa kikristo ni okoka kwa kukata shauri kumwomba Yesu awe mwokozi wako hapo ulipo(Biblia Yohana 3:16-21,36; Warumi 10:8-17; Matendo 16:31). Ukiita Mungu Baba katika jina la Yesu connection ya mbinguni unaipata mara moja. Hii itakuingiza kwenye ufalme tofauti. mkatae shetani na ujiweke kwa Mungu (Soma Biblia Yakobo 4:7). Kama umeingia maagano yoyote huko yakatatae na umuombe Mungu akusaidie kuyavunja uwe huru. Kama unachochote ulichochukua huko usiendelee kuwa nacho kitakusumbua(Matendo 19:18-20;). Mwanadamu anamsamaha wapo waliowekwa huru ni watu wa maombi na kusoma neno, Mungu anawashindia. Hii ni vita ya kiroho inahitaji maombi kwa yoyote anayetaka kuwa huru.

    ReplyDelete
  16. Mi nakushauri huu ujumbe peleka blog ya u turn kwa mange kule utapata watu wengi zaidi wa kuchangia. Blog ya michuz imekaa kihabari habari serious hivi.

    ReplyDelete
  17. Hakuna kitu kama icho hii habar ya kubuniwa tu

    ReplyDelete
  18. hahhaha yaani kuna watu wapumbavu sana yaani huyu bwege wa kiume anajifanya msichana na kubuni hadithi ya kijinga kabisa.halafu kuna majitu majinga eti mrudie yesu wako.mijitu inakimbilia yesu yesu kwa hadith ya kubuni.hahahhahahah

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...