Misaada ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya. 
 Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza. 
 Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo. 
 Kwa niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo aliouelekeza kwa mzazi huyo. Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila kona ya dunia. 
 Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
nasi tutafikisha ubani wako. 
Serengeti Freight wametoa ofa ya 
kusafirisha bure misaada ya aina hii 
ASANTENI SANA
Michuzi Blog/Mbeya Yetu Blog

Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.


 Misaada kwaajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya mara baada ya kufikishwa katika makao makuu ya Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure toka Uingereza na Wazee wa Kazi Serengeti Freight.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. daaaa ingekuwa ni mimi ninefurahi kama huo ni uzao wa kwanza maana mtu usingehitaji kuendelea kuzaa tena.

    ReplyDelete
  2. DIASPORA HUYOOOOO ANASAIDIA KUTOKA MAJUUUU JEEE WAZAWA MNAOPINGA URAIA PACHA MBONA HAMJITOKEZI KUMSAIDIA MT MWENENU??? UNADHANI HUYU AKIULIZWA KUHUSU SWALA LA URAIA KWA WA TA WAISHIO NJE KUPEWA HAKI YA KUINGIA NA KUTOKA ATAJIBU NINI??? NIMEONA WATU WEEEENGI WAMESHIKILIA MISIMAMO ETI HAWATAKI KUSIKIA WA TZ WAISHIO NJE KUWA NA HAKI YA KUWA NA URAIA WA HUKO NA WALIKO NA WAZIDI KUWA NA HAKI YA URAIA WA TZ PIA, WAKILETA HOJA YA NEGATIVE SIKUONA HATA MTU M'MOJA ALIEFIKIRIA KWENYE POSITIVE. HATA VITABU VYA DINI VILISEMA MWANAADAMU KAUMBWA KWA UBAYA %75 NA UZURI %25, NDIO MAANA MTU HAWEZI KUKUFIKIRIA VIZURI HATA KAMA ANAKUFAHAMU. SIWEZI KUWASHANGAAAA. LAKINI KULUMBANA KUSIKO NA TIJA HAKUTATUSAIDIA KWA HUU MCHAKATO BALI TUTAZAME HILI KWA UNDANI NA TUJIFUNZE KUTOKA NCHI ZILIZO KUBALI URAIA PACHA ZIMEATHIRIKA VIPI AU ZIMEFAIDIKA VIPI. ZIPO NCHI ZILIZOKUBALI URAIA PACHA KWA MIAKA ZAIDI YA 40 HATUJASIKIA UBAYA WA HALI HII HATA SEHEMU MOJA, ANZIA KWA JIRANI ZETU BURUNDI, RWANDA, KENYA, UGANDA NA UENDELEE NA KWINGINEKO KAMA NIGERIA, KAMEROOUN, GANA HATA NCHI ZA ULAYA KOTE URAIA NI KITU CHA KAWAIDA WALA HAKIWAKOSESHI USINGIZI.

    ReplyDelete
  3. Huhitaji kuwa raia pacha kuchangia mdau hapo juu. Ukiwa raia au sio raia utawatumia tu ndugu zako hela.

    ReplyDelete
  4. Wenzetu waliopo Bongo wanauchungu na sisi tulio nje! ukitaka kujua 'hate' zao wewe soma tu comments. ni hasira na chuki utafikiri sisi ndio mafisadi tunaoifilisi nchi.
    UK, Netherlands, Australia, New Zealand, Italy, USA ni miongoni mwa nchi zenye sheria za kuruhusu uraia wa nchi zaidi ya moja. Na ndio huko mabakuli ya kuomba misaada inakoelekezwa!

    ReplyDelete
  5. Jee wewe mtoa comment wa pili umesaidia nini katika kipindi chote uweko majuu? Umetoa mchango gani kwa kuisaidia Tanzania? Si unaendelea kuwaneemesha waliokuweka huko tuu kwa kuchangia pato lao la Taifa lao. C bado wanaendelea kukutumia tu hao kwa faida yao au hilo hulijuwi?

    ReplyDelete
  6. TATIZO LA NCHI YETU NI UKOMUNISTI ULIOJAA KATIKA VICHWA VYA VIONGOZI WA TAIFA HILI HATA URUSI NA ALBANIA WAKUBALI URAIA PACHA TANZANIA BADO WATAKATAA HII NDIO SHIDA YETU,NDIO MAANA HATA WAMAREKANI KILA MWAKA WANACHUKUA WAKENYA ELFU TATU NA WAGHANA ELFU ELFU MBILI NA KITU LAKINI TANZANIA NI MIA MBILI TU KATIKA ILE LOTTERY YAO KWA SABABU WANAJUA HAWA NI WAKOMUNISTI HUU NDIO UKWELI.
    NA WAKICHUKUA WATANZANIA WANATAFUTA WASIOSIDI MIAKA 25 KWA SABABU HAWA TAIFA JIPYA NA HAWAJUI UNYERERE TAFADHALINI MSIKASIRIKE HUU NDIO UKWELI MTUPU SASA KAZI KWENU TAFUTENI VISABABU VYA KIJINGA JINGA KUNA MBUNGE MMOJA WA CCM ALITAMKA KUWA URAIA PACHA HAPANA KWA KUWA WATAKULA HUKU NA HUKU SASA HUYU NDIO MBUNGE ALIECHAGULIWA NA WANA KIJIJI KAZI IPO KUWA N'GOA HAWA.
    MDAU.
    NAMIBIA.

    ReplyDelete
  7. Huyu mzazi ni mtoto sana. inaelekea hata mume hayupo!! Serikali impatie hifadhi na watoto wake kupitia Social Welfare Department. Hongerani sana wana Diaspora. Nachelea kusema vitu hivi vyaweza kuwa balaa kwake pamoja na kwamba haifahamiki ni nini kilichomo ndani. Ujangili hauchagui.

    ReplyDelete
  8. Wewe mdau #5 unayeuliza mwenzako ameifanyia nini Tanzania? Ngoja nikujibu,lakini si mie niliyesema ilo. Jamaa wakijitangaza wamefanya hiki mnasema wanapenda sifa au wanatafuta umaarufu(wanalinga).Na kila mtu aliye majuu siyo kusema ana uwezo wakusaidia kwa vile yuko majuu,majuu sio mbinguni. Nina uhakika asilimia 95% ya Watanzania walioko Ughaibuni wanachangia maendeleo ya TZ kwa kuwaletea ndugu zao pesa za matumizi ambazo zinaongeza mzunguko wetu wa hela Bongo. Ndiyo maana mnaona viongozi wanachukua waandishi wa habari kwenye kila kasherehe,maana wanajua mtauliza maswali kama haya. Maswali kama haya ni kushindwa hoja, tufikirie vitu vya maendeleo ya kweli. Mfano hao jamaa wa Ughaibuni wanaongezea nini kwenye maendeleo ya TZ?, iwe elimu, kuwekeza, utalaamu fulani,michezo na kadhalika. Tuache kufikiria kimasikini. Jamaa wa Ughaibuni ni plus kubwa kwa Bongo, huko waliko tu wanaitangaza TZ kwani watu wanauliza unatoka wapi na wanasema TZ. Watu wanauliza TZ inajulikan kwa nini?, wanajibu wanyama pori, Kilimanjaro, Tanzanite n.k Mtu huyo anakuwa amefanya kitu kikubwa kwa TZ.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...