Kampuni
ya bia ya Tanzania (TBL) kwa ushirikiano na Baraza la Sanaa Tanzania
(BASATA) leo tumezindua rasmi msimu mwingine wa Tuzo za Muziki Tanzania
zinazojulikana kama KTMA.
Mkutano
na wana habari za michezo na burudani kutoka vyombo mbali mbali ndio
umezindua msimu huu katika hoteli ya Kebby’s ilioko maeneo ya Mwenge
jijini Dar es Salaam. Viongozi wa BASATA pamoja na wa bia ya Kilimanjaro
walizungumzia mabadiliko chanya katika mchakato wa mwaka huu ikiwa ni
juhudi na hatua za kuendelea kuboresha mfumo wa upatikanaji wa wateule
wa vipengele mbali mbali vya tuzo hizi.
Mabadiliko:
Mwaka
huu watanzania wamepewa fursa ya kupendekeza wasanii, nyimbo, vikundi,
watayarishaji, video n.k wanazodhani zinastahili kuwepo kwenye mchakato
wa kuwapata wateule wa tuzo za muziki Tanzania. Kwakutumia mfumo wa SMS
na mtandao wapenzi wa muziki wataweza kutoa mapendekezo yao kupitia;
a. Namba ya simu 15440.
b. Mtandao – Website/tovuti na barua pepe/email.
Semina
fupi ilioendeshwa katika hoteli ya Kebbys ilitoa ufafanuzi wa jinsi ya
kutoa mapendekezo na wapi mpenzi wa muziki anaweza kwenda kupata maelezo
ya ziada yanayohusiana na njia za kutumia kupendekeza kazi na wasanii
wanaowataka.
“Baada
ya tathmini ya mwaka jana, tumeonelea wakati wa kuwahusisha wapenzi wa
muziki umewadia. Tuzo za muziki ni mchakato endelevu unaoendelea
kubadilika kila mwaka ikiwa ni jitihada za kuboresha na kuhakikisha
mfumo unakua imara, kuhakikisha tunapata wateule na washindi
wanaostahili’. Alisema George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro.
‘Kama
una amini msanii unaempenda ama kikundi ama wimbo n.k inastahili
kuingizwa kwenye mchakato, basi pendekeza.’ Alisema George.
BASATA
waliwapongeza TBL kwa kuendelea kuwa wabunifu na kuwa makini na
tathmini pamoja na taarifa mrejesho (feedback) za wapenzi wa muziki na
kuendelea kuzifanyia kazi alimradi kuboresha mfumo mzima wa tuzo hizi za
kitaifa.
“BASATA
ilipewa nafasi ya kutathmini mchakato huu mpya na tumeuridhia na
kuonelea ni mfumo mzuri wenye tija na utakaoleta matoke mazuri zaidi kwa
mchakato wa tuzo hizi.” Alisema mwakilishi wa BASATA.
Taarifa kamili za njia ya kupendekeza zipo kwenye mtandao wa Kili http://www.kilitime.co.tz/ktma pamoja na page ya facebook ya Kilimanjaro na kwa taarifa unaweza kuifata handle ya kili @kilimanjarolarger kwenye twitter.
Usiku wa tuzo unatazamiwa kuwa ni tarehe 3-Mei-2014 katika ukumbi wa Mlimani City.
Kwa
taarifa zaidi wasiliana na wasimamizi wa taarifa na mchakato wa KTMA,
1Plus kupitia anuani ilioainishwa hapo chini au na George Kavishe,
meneja wa Kilimanjaro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...