Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Lizzy Lloyd akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Mhe. Lv Youqing akitoa neno la shukrani kwa Benki ya Standard Chartered kwa kuandaa hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza kwenye halfa ya kuadhimisha mwaka mpya wa China, iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered na kufanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro, Dar es Salaam. Wakati wa hafla hiyo Balozi Gamaha aliupongeza Ubalozi wa China katika kusaidia na kuchangia maendeleo ya Tanzania. Pia Balozi Gamaha aliipongeza Benki ya Standard Chartered kwa kushirikiana na Ubalozi wa China nchini katika kurahisisha biashara kati ya Tanzania na China.
Wageni waalikwa walioshiriki hafla hiyo.
Balozi Gamaha akizungumza na Waandishi wa Habari.
Balozi Gamaha (kulia) akimsikiliza Bw. Nathaniel Kaaya, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa hafla hiyo. Wengine wanaosikiliza kutoka kushoto ni Bw. Iman Njalikai na Bw. Emmanuel Luangisa, Maafisa Mambo ya Nje.Picha na Reginald Kisaka
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...