Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Jenista
Mhagama (MB) akikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. George R.W. Nyatega (kushoto)) katika Ofisi za
Bodi hiyo zilizoko Mwenge, Dar Es Salaam .
Mh.Naibu Waziri akipeana mkono na baadhi ya
wawakilishi wa Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Naibu Waziri Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) wakiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Nyatega,
wakifuatilia mada ya Utoaji Mikopo iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Uchambuzi
na Utoaji Mikopo Bw. Onesmus Leizer (hayupo pichani)
![]() |
Naibu Waziri alipata pia bahati ya kukutana na mmoja
wa wanafunzi wake Bi. .Sarah Fihavango ambaye kwa sasa ni Afisa Mikopo
Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
----------
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ametembelea
ofisi za makao makuu ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yaliyopo
barabara ya Sam Nujoma Mwenge Dar Es Salaam.
Ziara
hiyo inafuatia uteuzi wake uliofanywa hivi karibuni na Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe.Jenista
Mhagama(Mb), ameipongeza Menejiment ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu kwa utendaji wao wenye ufanisi ulioperekea migomo kupungua katika vyuo
mbali mbali nchini, aidha Naibu Waziri amepongeza pia jitihada za Bodi ya
Mikopo inayofanyika katika urejeshwaji ambayo imeperekea kupatikana kwa Bilioni 19, ambazo pia zimetumika katika
ukopeshaji wa Wanafunzi wahitaji katika mwaka wa masomo 2013/14.
Katika
ziara hiyo Mhe. Naibu Waziri aliambatana na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Prof. Sylivia
Temu.
Akimtambulisha
Naibu Waziri kwa Menejimenti ya Bodi ya Mikopo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Bw. George Nyatega alisema ``……ni bahati
kutembelewa na Naibu Waziri ambaye bado ni mpya kwenye Wizara, kwani ni majuzi
tu ndiyo Mhe. Mhagama ameteuliwa katika
Wizara hii’’.
Aidha,
Bwana Nyatega alitumia fursa hiyo kumwelezea Naibu Waziri shughuli za kila siku za Bodi ya Mikopo ikiwa ni pamoja na historia
fupi ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo, mafanikio, na changamoto zinazoikabili
Bodi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...