Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akifungua kikao kwa maombi katika baraza la madiwani lilofanyika mwishoni mwa wiki kushoto ni naibu meya Gervas Ndaki na kulia Mkurugen Theresia Mahongo kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa. (picha na Denis Mlowe)
Juu na chini ni Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiwa katika kikao cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri mwishoni mwa wiki.
Habari na picha na Denis Mlowe
MIONGONI mwa watu 6003 mkoani hapa waliopima afya zao kwa hiyari katika kipindi cha Oktoba hadi Disemba mwaka jana, watu 379 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).
Akizungumza katika kikao cha utekelezaji wa shughuli za ukimwi zilizotekelezwa na Kamati ya Kudhibiti Ukimwi mbele ya baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya pili Oktoba na Disemba mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naibu Meya Gervas Ndaki, alisema kati ya waliojitokeza kupima na kupata ushauri nasaha, wanaume walikuwa 3074 wanawake 2,929.
Ndaki alisema kati ya watu 379 waliopima kwa hiari na kukutwa na maambukizi,146 ni wanaume na wanawake ni 233.
Alisema huduma ya kuzuia maambukizi ya vvu/ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, wajawazito 1,287 walijitokeza na kupata ushauri wa nasaha na kati yao, 84 sawa na asilimia 6.5 walikutwa na maambukizi.
Ndaki alisema mapambano ya ukimwi yanaambatana na huduma za tiba sahihi ya magonjwa ya ngono na jumla ya watu 361, wanaume 110 na wanawake 251, walipata tiba sahihi ya magonjwa ya ngono.
“Maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi yanaendelea kuwepo na tunajitahidi sana kuwahamasisha wananchi kujitambua na kutumia sana kondom na pia tumefanya sana kampeni kwa wananchi wanaotakiwa kwenda tohara kujitokeza kwenda katika hospitali na vituo vya afya vinavyotambulika kutoa huduma ya tohara” alisema Ndaki
Aliongoza kuwa huduma ya kitabibu ya tohara kwa wanaume ilitolewa kwa jumla ya wanaume 171 walitahiriwa na kati ya waliopima vvu wanaume 160 na hakuna aliyekutwa na maambukizi.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi aliwataka watendaji kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa kuwasisitiza wananchi kwa kuwapa elimu kuondokana na maambukizi mapya.
alisema mkoa wa Iringa una nafasi kubwa sana wa kuwa wa mwisho kama kila mmoja atatumia nafasi yake kuelimisha vijana kwa wazee katika mapambano dhidi ya ukimwi.
Kasi ya Maambukizi ya VVU inatisha!
ReplyDeleteNi wakati sasa wa Wanandoa kuwa na Ubunifu wa kuchonga chupi za mbao (Mbili kwa kila Kaya, Mume na Mke).
Mkitoka asubuhi mnapachika Kufuli zenu kila mmoja na njia yake, na kuja kufunguliana Kufuli jioni mkirudi.
Bila ya Mwamko wa Ubunifu huo (wa chupi za mbao), idadi ya Miji ya Makaburini itaizidi Miji ya Makazi ya kawaida ya nyumba zetu,
Woi, woi, woi, woi, maweee tutakwisha, tutakufwaaa!