Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana (wa tatu kulia) akipatiwa maelezo wakati akikagua utoaji wa mafunzo katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Munguri, Kondoa, akiwa ameambatana na Uongozi wa Wilaya ya Kondoa.

Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana akiwa katika ziara hii ya Kikazi alipata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Munguri, kondoa ambacho ni miongoni mwa vyuo 55 vinavyotoa mafunzo ya elimu ya wananchi, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya ufundi stadi, VETA.

Wakati wa ziara hii Mhe. Naibu Waziri aliiasa jamii ya Kondoa kutumia fursa hii kuwahimiza vijana kuja kupata mafunzo na ujuzi mbalimbali utakao wawezesha kujiajiri na hatimae kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, na hata kiwango cha umaskini katika jamii.

Alisisitiza kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuimarisha utoaji mafunzo katika chuo hiki na vingine nchini, ili kufikia vijana wengi zaidi na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM ya mwaka 2010.

Mh. Pindi Chana akisikiliza maelezo kwa vijana wanaochukua mafunzo ya ushonaji nguo katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Munguri, Kondoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...