Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Florence Turuka akitangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum la katiba   jioni hii katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jioni hii jijini Dar es salaam.
Wanahabari wakimsikiliza  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mhe.  Florence Turuka akitangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum la katiba  yakitangazwa jioni hii katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam. Bunge la Katiba litakalokuwa na wajumbe 640, litakutana kwa siku 70 (na kuongezewa siku 20 kama hawatoafikiana)  kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Desemba 30, mwaka jana. 
Kupata orodha kamili ya majina hayo  BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. The mdudu, haya sasa kumekucha ndugu zanguni mliochaguliwa msituangushe tunataka kuona tanzania mpya yenye kuchapa kazi na kuleta maendeleo ya ukweli,,wote mliochaguliwa TANZANIA KWANZA,,MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOOOTEEEE,the mdudu yuko njiani anarudi coz home ni home nishachoshwa na ubaguzi usio na kikomo,

    ReplyDelete
  2. Wanadiaspora hii imekaaje? Mbona sisi hatuna mwakilishi?

    ReplyDelete
  3. Hongera kwa kutambua hilo kaka, bora rudi home hata ukila mchicha lakini ni nyumbani. Mungu akubariki.

    ReplyDelete
  4. Kwa anayefahamu vizuri haya masuala:Watakuwa na SPIKA mpya?au wataongozwa na Spika wa JMT?Naomba achaguliwe Spika wa Bunge la Katiba na wasaidizi wake wa kuliendesha kwa hicho kipindi"It could just be a train coming in the other direction!"

    David V

    ReplyDelete
  5. kwa naoni yangu hilo bunge maalumu liwe makini hasa kuhusu serikali tatu kama mbili zimetushinda tutaweza tatu hata zingekuwa serikali tano kawaida ya muungani selikali ni moja kama uzalendo hakuna bora ibaki kama ilivyo chamsingi angalieni wapi panalalamikiwa mtafute ufumbuzi miaka hamsini ya uhuru hakuna wizara iliyosimama kwa miguu yake. tatueni matatizo ya wananchi wawekezaji bwelele rasilimali kibao bado mnayumba swala si kuongeza selikali kuweni wazalendo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...