Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu Dkt William Mgimwa, akiongea kwa niaba ya familia wakati wa mazishi ya baba yake kijijini Magunga jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Na Francis Godwin, Iringa

Mtokeo  ya  kura  za maoni  ndani ya  CCM yametangazwa usiku wa kuamkia leo  huku mtoto wa aliyekuwa mbunge  wa  jimbo hilo Godfrey Mgimwa akishinda kwa  kishindo  katika  nafasi hiyo, akifuatiwa na Jackson Kiswaga katika matokeo hayo.

Godfrey Mgimwa amepata  kura 342 huku Kiswaga  akipata kura 170 na mkuu wa wilaya ya Pangani Hafsa Mtasiwa akiambulia  kura 42 .

Matokeo hayo  yaliyotangazwa  katika  ukumbi wa shule ya  sekondari  Mwembetogwa mjini Iringa yanaonesha mgombea Peter Mtisi kapata  kura 33, Msafiri Pangagira kura 8, Bryson Kibasa kura 7, Edward Mtakimwa kura 3 na Thomas Mwiluka akiambulia kura 2

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kurithiana hata uongozi..mmh hii naona haijakaa vizuri.

    ReplyDelete
  2. Kwaht hata wapiga kura wamerithiwa? Unless useme kama mzazi akiwa kiongozi mtoto asiwe kwa namna yoyote, kitu ambacho kitakua kicgekesho@salum said

    ReplyDelete
  3. Safi sana kijana..kwani shida ni nini?? acha wivu wewe anon.

    ReplyDelete
  4. Kura ra huruma hazitoleta maendeleo ya kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...