AFISA MSAMBAZAJI WA
TANROAD AFARIKI
DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI MKOANI MBEYA.
GARI LISILOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE
LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI AITWAYE ANDREW
CHIWINGA (50) AFISA MSAMBAZAJI WA
TANROAD NA MKAZI WA IWAMBI MBEYA ALIYEKUWA ANAENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI STK 8793 AINA YA TVS STAR
NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 08.02.2014 MAJIRA YA SAA 20:45HRS USIKU ENEO LA IYUNGA
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
DEREVA ALIKIMBIA PAMOJA NA GARI
MARA BAADA YA TUKIO HILO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...