Na Abdulaziz Ahmeid,Kilwa Masoko
Familia moja ya Bw Bernad Towele dereva wa Gari la Takukuru Wilayani
Kilwa Imenusurika baada ya Nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea
kwa moto usiku wa kuamkia katika mji mdogo wa kilwa masoko.
Akithibitisha kutokea kwa tukio la Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa
6 usiku kuamkia leo,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,Joseph
Mfungomara alieleza kuwa chanzo cha Moto huo bado hakijajulikana ila
hakuna majeruhi.
Kamanda Mfungomara alimalizia kuwa Vitu vyote vilivyomo katika nyumba
hiyo vyenye thamani ya Tshs 7,700,000/ Havikuweza kuokolewa.
Baadhi ya Wananchi waliopo katika mji huo Akiwemo Mfanya biashara
Ahmaid Shukra na Saidi Timamy mmiliki wa kituo cha Mafuta cha Alsat wameiomba Halmashauri hiyo kupeleka ombi
maalum serikalini ili waletewe gari la Zimamoto kutokana na wilaya
hiyo kuanza uwekezaji unaotokana na Raslimali ya Gesi ya Songosongo
pamoja kukua kwa mji huo mashuhuri Afrika ya Mashariki
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...