Pichani wa tatu kulia ni  Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa Kampuni ya Angels Moment ya jiji Dar,akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ya Serena Hotel,kuhusiana  tamasha la kwanza na la aina yake kufanyika nchini Tanzania, lenye lengo la kuongeza na kuchochea uelewa wa wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiwekea akiba.

 “Tamasha hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada na maonesho,” alisema Bi Pamela. Pichani kulia ni Meneja  Mawasiliano wa kampuni ya Angels Moment,Bi.Beatrice Millinga,Mratibu wa Matangazo na Mahusiano kutoka kampuni ya AZAM/Bakharessa,Bwa.Mohameda Ramadhani (Mdhamini wa tamasha hilo),pamoja na mwisho kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo kutoka kampuni ya MONTAGE LTD,Bi,Teddy Mapunda.
Pichani ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Angels Moment ya jiji Dar wakiwa katika picha ya pamoja,mara baada ya mkutano kumalizika.
========  ======= =========
Na Beatrice Millinga
Kampuni ya Angels Moment ya jijini Dar es Salaam imetoa wito kwa wadau wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo kujitokeza na kudhamini tamasha la kwanza la kipekee kwa ajili ya wanawake na vijana lililopewa jina la Mwanamke na Akiba na linalotarajiwa kufanyika kuanzia Februari 19 - 21, 2014 kwenye Ukumbi wa  Dar Live - Mbagala, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa wahabari katika ukumbi wa Serena leo, Mkurugenzi wa Habari na Matukio wa Kampuni ya hiyo, Bibi Pamela David amesema kuwa makampuni na mashirika mbalimbali yatapata fursa ya kujitangaza,  na kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao kwa wanawake na vijana wa Kitanzania.
“Kwa kudhamini Tamasha hili wadau watapata sio tu fursa ya kutangaza biashara na huduma zao bali kujitangaza wao wenyewe na kutoa elimu kwa umma maana si wananchi wote wanauelewa wa huduma zitolewazo na mashirika na makampuni mbalimbali hapa nchini,” alisema Bi Pamela.
Kwa mujibu wa Bi Pamela, Tamasha hilo ni la kwanza na la aina yake kufanyika nchini Tanzania lenye lengo la kuongeza na kuchochea uelewa wa wanawake katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiwekea akiba.
“Tamasha hili limeandaliwa ili kuwaonesha wanawake na vijana umuhimu wa kuweka akiba, aina tofauti za kuweka akiba na njia mbalimbali za kuweka akiba pamoja na fursa za kuweka akiba kimkakati kupitia uwasilishaji wa mada na maonesho,” alisema Bi Pamela.
Aliongeza kuwa washiriki watapata fursa ya kupata elimu juu ya kukabiliana na hatari katika uhifadhi wa fedha na masuala mbalimbali yahusikanayo na usimamizi wa fedha.
Akizungumza mfumo utakaotumika kuendesha tamasha hilo, msemaji wa kampuni, Bi Pamela alisema “Tamasha litakuwa kwenye mfumo wa maonesho pamoja na vipindi vinne vya uwasilishaji wa mada mbalimbali toka kwa wanawake wafanyabiashara waliofanikiwa na wataalamu waliobobea kwenye nyanja hizo.
Kwa mujibu wa msemaji huyo watoa mada wanaotarajiwa kuwasilisha ni pamoja na Naibu Gavana Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Natu Mwamba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)  Bibi Irene Isaka.
Tamasha linatarajia kuwavutia washiriki 5,000 na waonyesha bidhaa 50 kutoka maeneo mbalimbali katika sekta ya usimamizi wa fedha. Pia, inatarajiwa kuvutia washiriki toka sekta nyingine ikiwemo biashara zenye mahusiano na suala zima la uhifadhi wa fedha na uwekaji wa akiba kwa wanawake.
Mgeni rasmi wa Tamasha hili anategemewa kuwa Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal.
Mualiko wa Mama Asha kwenye Tamasha hili unachagizwa na ujasiri na mchango wake, pamoja na kujitoa kwake kwa hali na mali katika kusaidia wanawake, vijana na makundi mbali mbali yenye uhitaji nchini Tanzania.
Tamasha limedhaminiwa na Said Salim Bakhresa (SSB), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Benki ya CRDB, STANBIC, FINCA, Mamlaka ya  Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko Ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Wadhamini wengine ni pamoja na Mfuko wa UTT, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) na Kampuni ya Ashton Media.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...