Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye akiwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma tayari kwa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili.
 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa akizungumza na Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye kabla ya kuanza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma.
 Ndugu William Ngeleja akisubiri kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama.
 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa kizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo alisema mazungumzo yalikuwa mazuri,yalikuwa yenye nia ya kukijenga chama kwa ajili ya uchaguzi 2015.
Waandishi wa Habari wakiwajibika kuandika habari nje ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi ambapo viongozi watatu walihojiwa na Kamati ndogo ya Maadili.

Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula  leo imewahoji watu watatu ambao wawili walishawahi kuwa Mawaziri Wakuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. 
Mawaziri hao waliohojiwa leno ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa,Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema Ndugu William Ngeleja ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
 Kamati hiyo bado ina kazi ya kuwahoji viongozi wengine watatu ambao leo walishindwa kufika baada ya kuomba hudhuru kwani walikuwa na majukumu mengine ya kiserikali.
Ambao hawakufika leo ni Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe ambaye yupo safarini nje ya nchi ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen Wassira na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. The mdudu,,anasema CCM inakoelekea nikule kwa enzi za mpendwa wetu Nyerere(RIP) hii safi sn coz haogopwi mtu hiyo ndio misingi imara ya chama chochote,coz chama ni sawa na MBABA Wenye watoto zaidi ya 15 kwenye hao watt akiona baadhi yao wanaanza kumjadili mitaani eti oo baba sikuhizi hampendi mamaetu wakati sikweri,,sasa hizi habari zikivuja mpaka zimfikie baba yao atakacho kifanya ni hiki hapa ndugu wadau wa Michuzi,moja atawaita wale watt wake watukutu wenye nia ya kuleta mtafaruku pale nyumbani kwao MBELE ya MJOMBA,BIBI,SHANGAZI,ili wajieleze vizuri na kueleweka,so hivyo ndivyo walivyofanya CCM,the mdudu hana chama ila anaona mbali sn na mijiakiri aliojaariwa na MUNGU WAKE,,siku njema kwenu woote ni hayo 2 kwa leo

    ReplyDelete
  2. Kiswahili chako hakipo vizuri wewe ni raia wa kongo nini?

    ReplyDelete
  3. The Mdudu habari yako bwana na za mwaka mpya!?. Leo umenivuta hadi nikaseme nisipite bila toa cooment zangu japo kwa uchache tu.
    Popote pale ulipo ndugu yangu umesalimika na SNOW YA MWAKA MPYA? Kwa kweli leo The Mdudu umenivutia na kutambua kumbe kweli wewe ni Mzalendo kwa kunirejesha kule kwenye kusimamia maadili ya kweli zama zilee za Mwalimu JK NYERERE (RIP).

    Personally kitu hiki kimenivutia sana cha chama chetu kuamua kuwaita hawa majamaa wenye UROHO na UCHU WA MADARAKA kwenda kule kujieleza kwa kuanza campaign kabla ya wakati huku wakiwa hawana uhakika kama wao ndo chaguo halisi la chama chetu.
    Kusema kweli ukiukwaji na uvunjifu wa kanuni ni kitu hatari sana. Ikiwa kama leo wewe ni mwananchi tu au kiongozi mdogo wa ngazi ya UBUNGE na UWAZIRI unafikia hatua ya kuvunja kanuni na kuanza campaign kabla ya wakati je! tukikuweka pale IKULU itakuwaje?
    Tukishakupa URAIS si ndo itakuwa balaa kubwa jamani?
    Watanzania wenzangu na wale viongozi ambao tumewapa dhamana ya kututawala kwa sasa ni muhimu kanuni zitumike kuwaadhibu hawa walioanza campaign kabla ya wakati. Ikitokea mmoja miongoni mwa hawa akapitishwa kuwa mgombea wa uraisi hamuoni mtakuwa mmetupa mashaka makubwa? MAJINA YA LOWASSA, SUMAYE, MEMBE, NGEREJA na MAKAMBA must be removed from the list ya wale watarajiwa hiyo ndo inapaswa kuwa adhabu yao ya kwanza.

    The Mdudu kwa kuwa umenifurahisha kwa kuutambua umahili wa Mzee wetu JK Nyerere napenda kuwarejesha nyuma kwenye moja ya kauli zake ambazo alikuwa akisisitiza na kutuasa saaana.
    Mwalimu alisema " HIVI KULE IKULU KUNA BIASHARA GANI YA KUKIMBILIWA?, WEWE UNAYETOA MAPESA MENGI ILI UENDE IKULU HIVI KUNA BIASHARA GANI PALE YA KUKIMBILIA HATA UTOE MIJIPESA?, JINSI GANI UTAREJESHA HIYO MIJIPESA UNAYOTUMIA ILI UINGIE PALE IKULU?.
    Mwalimu akatuasa pia " MTU ANAYEKIMBILIA KWENDA IKULU NI MTU WA KUMUOGOPA KAMA VILE UKOMA"

    Hapo THE MDUDU na Watanzania wenzangu tunajifunza nini? Kusema kweli Mwalimu alikuwa a visionary leader na aliona mbali sana. Aliyoyasema miaka ileee leo tunayaona na tukiyapuuzia tutaangamia vibaya.
    Watu wameanza campaign kabla ya wakati na wengine wanadiriki hata kutoa "mijipesa" kibao eti wakiita ni HARAMBEE, hivi kweli harambee katika kipindi hiki kwa nini? ulikuwa wapi kufanya harambee tokea wakati wote? Hizi pesa unazochangia na kuzitoa zinatoka wapi? KAMA ni zako umezipata KIHALALI?, tunaweza pewa financial record yake? zinalipiwa kodi?. Kama ni MKOPO hebu tuelezwe anayekukopesha terms zake ni zipi?, UTAZIREJESHA vipi ukishafika pale IKULU? Kwa nini unakimbilia pale??? IKULU haikimbiliwi na wala hainunuliwi kwa MAPESA wanaokupa mapesa kama ni marafiki zako utawarejesheaje hizo pesa? tuwe makini tusijejikuta tunauza nchi yetu hivi hivi kwa MIJITU ambayo niya yao siyo kujenga bali ni kujitajirisha yenyewe.

    The MDUDU wewe huna affiliation na chama chochote, Mimi ni CCM DAMU na kusema kweli chama chetu kujisafisha lazima KANUNI NA MAADILI YASIMAMIWE ili tuweze kuwa tunakwenda na karne ya 21. Asiogopwe mtu eti kwa sababu ya MIJIGUVU yake au MIJIPESA yake bwana. UZALENDO na ETHICS lazima zitumike na ni vyema hawa watu wote waenguliwe na wasisimame tena kwenye ugombea wa urais 2015 na asiogopwe mtu kabisaaa.
    Waelezwe mmevunja kanuni na hivyo adhabu tunaondoa majina yenu wawe " BLACKLISTED" na kama wanataka kwenda kwenye chama kingine wapewe " RUKHSA" sioni kama kutakuwa na mtikisiko wowote kuliko kubeba watu wachafuzi kama hawa.

    Mheshimiwa MANGULA nakufahamu tokea MWANZA na najua umakini wako katika kusimamia HAKI na USAWA hivyo hawa jamaa wafanyie kazi na isiishie kwenye kablasha za ofisini MAAMUZI yawekwe wazi Watanzania wenye NIYA safi wajue kinachoendelea na mkifanya otherwise kwa kuogopa nguvu zao you will be digging your own grave.

    Nahitimisha kwa kusema " ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA CCM na KIDUMU CHAMA CHETU MAKINI na TUZIENZI HEKHMA ZA WAANZILISHI WAKE ili KUKINUSURU.

    ReplyDelete
  4. Uncle Michuzi naomba mada hii uirejeshe tena juu ili Wadau wachangie zaidi.

    ReplyDelete
  5. Ni jambo zuri sana na jambo la kukijenga chama.CCM siku zote ni chama makini na chama madhubuti na kipo kwa ajili ya waTanzania wote. Tunapongeza sana kwa utaratibu wa kuwaita viongozi wetu na kupeana mikakati ya kukiimarisha chama.Ahsante sana na penda kuwasilisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...