Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiashiria jambo wakati wa akiufunga mkutano wa Tafakuri na maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania katika ukumbi wa White sand jijini Dar es Salaam,uliowashirikisha wanasiasa,Mashirika ya Kijamii na Viongozi wa Dini mbali mbali nchini
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa siku mbili kuhusu tafakuri na maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiufunga mkutano uliowashirikisha watu mbali mbali wakiwemo Wanasiasa,Viongozi wa Dini na Mashirika ya Kijamii Nchini
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi katika Hoteli ya Whitesand Jijini Dar es Salaam,kuufunga mkutano wa siku mbili wa Tafakuri na maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania pia Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Joseph Mbatia baada ya kuufunga mkutano wa siku mbili wa Tafakuri na Maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania,Ukumbi wa Whitesand Jijini Dar es Salaam leo jioni. Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...