|
Polisi wamemakamata mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard (wa nne kushoto) wakimtuhumu kupiga picha mahakamani. Hadi sasa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi huku kesi ya mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi ikiendelea kusomwa.
Habari mpya zinasema askari wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa wamemwachia huru Frank Leonard aliyekamatwa ndani ya chumba cha mahakama wakati akifuatilia mwenendo wa kesi ya mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Marehemu Daudi Mwangosi.

Polisi hao wamemwachia huru Leonard baada kwa kile kinachosadikiwa kutokuwa na ushahidi kuwa amepiga picha mahakamani wakati mtuhumiwa wa mauwaji hayo ambae ni askari polisi akisomewa mashtaka yake.
Mwanahabari huyo amesema yeye hakuwa amewasha kamera yake mahakamani hapo bali alikuwa ameshika simu yake kabla ya askari mmoja kusimama na kumkamata ndani ya mahakama wakati kesi hiyo ikiendelea.
SHERIA IPI INAZUIA KUPIGA PICHA MAHAKAMANI? AU KUNA ZUIO LOLOTE LA KISHERIA LIWEKWA? MANAKE DEMOKRASIA NI PAMOJA NA UHURU WA WATU KUJUA KINACHOENDELEA, YANI UWAZI
ReplyDeletewewe wa kwanza sema unachotaka kusema usibwabwaje tu. unadhani kila kitu sheria? Taratibu pia hufunga(bind) mtu. Upinzani kila kitu. Unaboa
ReplyDelete