Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.

Eneo hilo la Tengeru ambalo zamani lilikuwa likimilikiwa na Hortculture Tanzania Ltd linatazamiwa kujengwa mji wa kisasa utakaojulikana kama Satelite City.

Mkurugenzi wa shirika la nyumba la taifa NHC Nehemea Mchechu aliwaambia wajumbe wa kamati ya ardhi ,amaliasili na mazingira kuwa tayari NHC imenunua ekari 600 ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 5.

Nyumba 300 zinatarajiwa kujengwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo kadharika kutajengwa maduka makubwa ,shule pamoja na vituo kwa ajili ya huduma kwa jamii na kwamba ujenzi wa nyumba nyingine 300 utafuati.

Mchechu alisema ujenzi huo hauta athili kwa namna yoyete ile uoto wa asili ikiwemo miti katika eneo hilo na kwamba wanataegemea kuacha sehemu ya Mikahawa iliyopo hapo kama kumbukumbu.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu akisalimiana na mbunge wa jimbo la Arumeru Joshua Nassar wakati kamati ya bunge ya Ardhi ,maliasili na mazingira ilipotembelea eneo ambalo linatazamiwa kujengwa Mji wa kisasa ujulikanao kama Satelite City.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la taifa(NHC)Nehemia Mchechu akiteta jambo na mkurugenzi wa shirika la hifadhi la taifa(TANAPA)Allan Kijazi alipotembelea eneo ambalo linatazamiwa kujengwa Mji wa kisasa ujulikanao kama Satelite City eneo la Tengeru Arusha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...