Benki ya NMB imezindua tawi jipya barabara ya Mandela mkoani Dar es Salaam. Vilevile imetoa msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Amana.
Hili ni tawi la ishirini kufunguliwa katika mkoa wa Dar es Salaaam, na hii inafanya NMB kuwa benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania, ikiwa na matawi zaidi ya 150 yaliyosambaa nchi nzima.
Tawi hili la NMB Mandela Road, linatoa huduma mbali mbali za kibenki ikiwemo akaunti za akiba, mikopo , huduma za fedha za kigeni, kukusanya mapato na kulipia kwa niaba ya serikali na taasisi mbalimbali.
Tawi hili litakua wazi kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni ( 2:30 asubuhi - 10:30 jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (8:30 asubuhi- 6:30 jioni), Jumapili na siku za sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi hili.
Katika kusherehekea ufunguzi rasmi wa tawi hili, Benki ya NMB ilitoa msaada kwa jamii wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni kumi ili kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi katika kuboresha huduma katika sekta ya afya.
Msaada huu unatolewa kwa hospitali ya Amana pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadick akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa
tawi la NMB Mandela Road .Kwanza kushoto ni Meneja wa NMB kanda ya Dar es
salaam ,Bw. Salie Mlay na kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha
Huduma kwa wateja wakubwa NMB, Bw.Gerald Kamugisha wakishuhudia ufunguzi
huu uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
Meneja wa NMB kanda
ya Dar es salaam, Bw. Salie Mlay akimwelezea Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa
Dar es salaam (kwanza kushoto , Mhe Said Meck Sadick huduma mbali mbali zitolewazo na
tawi jipya la NMB Mandela Road
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Said Meck Sadick akiwa
katika picha ya pamoja na maafisa wa NMB tawi la Mandela Road.
Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam, Mhe Meck Sadick (kwanza Kulia) akimkabidhi sehemu ya
msaada wa vifaa vya hosipitali Mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana
,Dr Meshack Shimwela .Mashuka ya Hospitali pamoja na Vitanda vya wodi ya akina
mama ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa .Makabidhiano haya yamefanyika jana
wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB mandela Road Katikati ni Meneja wa NMB kanda
ya Dar es salaam, Bw.Salie Mlay.
Hivi barabara ya Mandela ilivyo paaana ina maana tumeshindwa hata kutoa location? Ni kweli hatuna addresses za kiviile lakini hata kusema eneo fulani ? maana tuanzie kuhisi kuwa ni Kurasini, Tazara, Buguruni, Matumbi au Relini?
ReplyDelete